1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Siku saba za maombolezo Zanzibar

17 Februari 2021

Serikali ya Zanzibar imetangaza siku saba za kuomboleza na bendera kupeperushwa nusu mlingoti kufuatia kifo cha aliyekuwa makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad.

https://p.dw.com/p/3pUPC
Sansibar Maalim Seif Sharif Hamad CUF Präsidentschaftskandidat
Picha: Getty Images/AFP/T. Karumba

Ni simanzi, majonzi na vilio vilivyotawala katika maeneo mwengi ya mji wa Zanzibar hasa katika mitaa ya Vuga Mji Mkongwe ambapo wafuasi wengi wa Maalim Seif wanaishi katika eneo hilo huku watu mbali mbali wakiendelea kumiminika katika ofisi za chama cha ACT Wazalendo.

Wazanzibari kumuombeleza Maalim Seif kwa siku saba

Muda mfupi baada ya ya Rais wa Zanzibar kulitangazia taifa juu ya kifo cha Maalim Seif watu wengi walikwenda kumfariji akiwemo mwanasiasa maarufu Mansoor Himid aliyekuwa mshauri wa Maalim Seif.

Wengi wanamzunguzia Maalim Seif kama kielelezo cha demokrasia na amesimamia vilivyo aliyokuwa akiyaamini katika uhai wake wote wa kisiasa hadi anamaliza pumzi zake za mwisho. Maalim Seif ametimiza ndoto yake kuu ya kuwaunganisha wazanzibari. Hassan Jani ni mmoja wa wanasiasa vijana anaeleza.

Maalim Seif anatarajiwa kuzikwa Alhamis mchana Kijijini kwao Matamwe Kisiwani Pemba. Mbuyu wa demokrasia Jumatano umeng'oka, hakika sote ni wa Mwenyezi Mungu na marejeo yetu ni kwake.