1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Siku ya muungano wa Ujerumani

Admin.WagnerD3 Oktoba 2014

Katika kuadhimisha miaka 24 ya muungano,25 tangu ukuta wa Berlin ulipoporomoka,kansela Angela Merkel amekumbusha yaliyotokea mwaka 1989,akashadidia hali ya kuishi pamoja wakaazi wa mashariki na magharibi pamoja

https://p.dw.com/p/1DPZh
Tag der Deutschen Einheit 2014 Hannover
Kansela Angela Merke katika siku ya kumbukumbu ya Muungano HannoverPicha: picture-alliance/dpa/P. Steffen

Vilevile na kuzungumzia kitisho kinachotokana na wanamgambo wa itikadi kali wa dola la kiislam IS.Waziri mkuu wa jimbo la Lower Saxony,amehimiza ukarimu kuelekea wahamiaji.Kuhusu sherehe za miaka 24 ya muungano zilizofanyika hii leo mjini Hannover anasimulia Oummilkheir.

Kansela Angela Merkel ametoa picha ya kuridhisha ya kuishi pamoja wajerumani baada ya muungano.Matumaini mengi yamekamilishwa,Ujerumani mashariki imefanya maendeleo makubwa" amesema kansela Angela Merkel katika sherehe za kuadhimisha siku ya muungano wa Ujerumani mjini Hannover.

Hali ya kisiasa dunani

Katika hotuba yake kansela Angela Merkel amezungumzia hali ya kisiasa inayoikabili dunia yetu hivi sasa,ikiwa ni pamoja na mzozo wa Ukraine,maradhi ya kuambukiza ya Ebola na pia mpambano dhidi ya wafuati wa itikadi kali wa Dola la Kiislam IS.

Tag der Deutschen Einheit 2014 Hannover
Kansela Merkel na viongozi wenginePicha: picture-alliance/dpa/O. Spata

Kansela Merkel ameongeza kusema anaetembea katika miji ya mashariki anatambua kwamba kuna mengi yaliyotekelezwa tangu mwaka 1990.Hata hivyo amekumbusha kuna mengi pia yanayohitaji kutekelezwa;idadi ya wasiokuwa na kazi bado ni kubwa kuliko magharibi,hata kama kwasasa idadi hiyo ni ya chjini kabisa kuwahi kushuhudiwa tangu muungano.

Kumbukumbu ya muungano

Sawa na kansela Merkel,waziri mkuu wa jimbo la Lower Saxony pia Stephan Weil wa chama cha SPD amekumbusha katika hotuba yake yaliyotokea msimu wa mapukutiko mwaka 1989 na kusifu ujasiri na ukakamavu wa wananchi wa GDR ya zamani wakati wa mapinduzi ya amani.Vuguvugu hilo la amani ndilo lililoplekea kuungana upya Ujerumani amesisitiza waziri mkuu wa jimbo la Lower Saxony.

Stephan Weil, ambae kutokana na wadhifa wake wa spika wa baraza la wawakilishi wa majimbo,nie aliyepewa dhmana ya kuandaa sherehe za mwaka huu za muungano amewatolea wito wajerumani wawe wakarimu kuelekea wakimizi."Wengi wa wakimbizi wa leo ndio wazakaokuwa majirani zetu wa kesho na hivyo ndivyo wanavyobidi kutendewa-amesisitiza.

Kansema Merkel kwa upande wake amelaani visa vya kudhalilishwa wakimbizi akisema wahalifu wanabidi waandamwe kisheria.

Kutokana na migogoro inayoikabili dunia wakati huu,kansela Merkel amesema litakuwa kosa kusalim amri.Kumbukumbu za mwaka 1989 1990 anasema zinaweza kusaidia kukabiliana na changamoto zilizozoko.

Sherehe za muungano wa Ujerumani zimeanza leo asubuhi kwa misa maalum katika kanisa la Martktkirche mjini Hannover.Katika uhubiri wake askofu wa kanisa la kiinjili Ralf Meister amekumbusha binaadam kote ulimwenguni ni wa moja mfano wa familia moja.Dini au asili visiachiwe kuwa sababu ya watu kutojuana.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Epd
Mhariri:Yusuf Saumu