1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Siku ya Redio Ulimwenguni

13 Februari 2013

Leo (13.03.2013) ni siku ya redio duniani ambako nchini Tanzania kunafanyika kongamano maalum linalowajumuisha waandishi habari, makundi ya wasomi, mashirika ya Umoja wa Mataifa na watetezi wa uhuru wa maoni

https://p.dw.com/p/17dIc
Eine Kundin betrachtet am Mittwoch (13.02.2002) in einem Hamburger Kaufhaus einen modernen Weltempfänger. Mit der Digitalisierung von Kurz-, Mittel- und Langwellen soll nach den Vorstellungen von Sendeanstalten und Industrie der sogenannte AM-Bereich im Hörfunk eine Renaissance erleben. ( Zur dpa-Reportage "Das Zauberwort heißt DRM - Klangerlebnis statt Knistern" vom 14.02.2002)
Weltempfänger (Sony)Picha: picture-alliance/dpa

Mjadala huo pamoja na kugusia maeneo mbalimbali, umezingatia pia kwa kiasi gani vyombo vya utangazaji vya umma vinawajibika ipasavyo kuwasiliana na wananchi bila kuwa na dhana ya upendeleo kwa dola zilizoko madarakani.

Wakati kukishuhudiwa utitiri wa vyombo vya habari ambavyo vimetapaa kila kona ya nchini, bado vyombo vya umma vinaendelea kufutiliwa kwa karibu na wananchi ambao wanahisi kuwa vinawajibu wa kukithi matakwao yao pasipo kuwepo kwa dhana yoyote ya upendeleo.

Watangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW
Watangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DWPicha: DW

Hivyo Wachangiaji wengi wengi kwenye mjadalo huo wamekosoa na kulaaumu namna ya utendaji kazi wa vyombo hivyo vya umma wakieleza kuwa, vinaegemea zaidi maslahi ya upande mmoja na kuyapa kisogo maslahi ya wananchi.

Kwa kiasi kikubwa vyombo vya habari vya umma nchini Tanzania vinazingatia zaidi kuteleleza matakwa ya dola na wakati mwingine vinaandamwa na makundi ya kiharakati kutokana na hulka za vyombo hivyo kutotoa fursa sawa kwa vyama vya siasa vya upinzani hasa panapojitokeza suala la uchaguzi Mkuu.

Akijadilia mada hiyo, mwanaharakati na mwandishi wa habari wa siku nyingi Ndimara Tigambwage, alilaumu juu ya mwenendo wa vyombo vya umma, ambavyo alisema kuwa wakati mwingine haviwajibiki ipasavyo.

Redio ni chombo muhimu katika kueneza habari
Redio ni chombo muhimu katika kueneza habariPicha: Conti-Press Heinz Fremke/Staatsarchiv Hamburg

Suala la gharama za uendeshwaji pamoja na mabadiliko ya mara kwa mara ya soko ni eneo jingine linalokwaza ufanisi wa vyombo vingi vya utangazaji nchini Tanzania. Hata hivyo baadhi ya wachunguzi wa mambo wanaona kuwa, bado vyombo hivyo vinanafasi ya kutumia fursa a mabadiliko ya kiteknolojia kukabili wimbi la ushindani.

Kwa upande wake, Bi Pil Mtambalike afisa kutoka Baraza la Habari, anaona kuwa, pamoja na mikwamo inayoendelea kushuhudiwa kwenye vyombo vya umma, lakini hali hiyo inaweza kurekebishika iwapo kutajitokeza utashi wa dhati.

Katika taarifa yake kuadhimisha siku hii ya redio duniani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon aliihimiza dunia kutumia sauti za mawimbi ya redio kuhimiza amani, upendo na ulinzi kw awatoto na kuzuia kujiri kwa migogoro.

Mwandishi: George Njogopa

Mhariri: Josephat Charo