1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Simba na Yanga wajiandaa kwa robo fainali

Saumu Njama Mhindi Joseph
25 Machi 2024

Maandalizi kwa wawakilishi wa Tanzania Simba na Yanga yameendelea kushika kasi Kuelekea michezo ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

https://p.dw.com/p/4e6Q6
Simba dhidi ya Al Ahly
Mechi kati ya Simba na Al Ahly katika uwanja wa Benjamin Mkapa - Dar es Salaam - Tanzania.Picha: Sports Inc/empics/picture alliance

Mnyama Simba atawakaribisha Al Ahly ijumaa ya Machi 29 huku wananchi Yanga  wataumana na Mamelodi Sundowns ya Africa Kusini Jumamosi ya machi 30.

Simba wamekita kambi Visiwani Zanzibar na wachezaji wa simba  kuelekea mechi hiyo wanasema "Naamini  Timu yangu itatinga nusu Fainali msimu huu kwa sababu  Al Ahly tumecheza nao miezi michache iliyopita na tunajua makosa Yao" alisema Golikipa wa Simba  Ally Salim.

"Mechi hiyo ni kubwa  tunahitaji matokeo naamini uwepo wa Mashabiki uwanjani utatupa nguvu ya kupambana" alisema David Kameta.

Kocha msaidizi wa Simba Seleman Matola anaelezea Hali ya Kambi ya simba kuelekea mchezo huo "Maandalizi  kiukweli yapo vizuri sana mechi yetu ipo usiku  tumekuwa kifanya mazoezi muda ule ule ambao tunaenda kucheza mechi ni wakati wetu wa kuweka Historia kwa kumvua Bingwa mtetezi  na  kwenda hatua ya Nusu Fainali kwa sababu tumekuwa tukiishia hatua ya robo fainali”alisema Kocha msaidizi wa Simba Seleman Matola.

Yanga imejipangaje?

Young Africans
Wachezaji wa Young Africans ya Tanzania Picha: Young Africans

Kwa upande wa Yanga ambao watavaana na Mamelodi Sundowns ya Africa Kusini Meneja wa Timu hiyo Walter Harrison  anasema "kikubwa ni kuiandaa Timu ili kuweza kuwa katika hali nzuri ya kiushindani kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwadhidi ya Mamelodi Sundowns na tutahakikisha kila kitu kinaenda sawa na  furaha kwa wananchi inarejea."

Mechi hizi zinasubiriwa kwa shauku kubwa kuona Simba na Yanga zitafanya nini wachambuzi wa soka wanatazamia hiki "Simba na Al Ahly ni mechi ambayo Al Ahly wanaweza kuingia kwa tahadhari kubwa kuliko mechi zote walizowahi kucheza na Simba kwa sababu wanafahamu katika uwanja wa Benjamin Mkapa Mara  mbili mfululizo hawajawahi kupata matokeo ya ushindi mechi zote zitakuwa ngumu kila Timu itakayojiandaa vizuri inaweza kupata matokeo”Alisema Hamis Makila Mchambuzi wa Soka Tanzania.

"Wapizani ambao wanakutana nao na aina ya Madaraja ambayo yapo na mafanikio yanga ananafasi kama atapambana licha ya Yanga kuzidiwa ubora  na Mamelodi Sundowns"Alisema Jastin  Mhalinga Mchambuzi wa Soka Tanzania

Katika misimu mitano iliyopita, Simba imeingia hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mara tatu huku ikifika hatua hiyo kwenye Kombe la Shirikisho Afrika mara moja na msimu huu wanasaka hatua ya Nusu Fainali.

Mindi Joseph