1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sio chini ya wapiganaji 40 wauwawa huku mapambano yakiendelea Islamabad

10 Julai 2007

Wapiganaji hao wameuwawa mapema leo baada ya vikosi kuvamia tena msikiti mwekundu kufuatia kuvunjika mazungumzo ya kutafuta suluhu

https://p.dw.com/p/CB2x
wakaazi wanaishi karibu na msikiti mwekundu wakimbia ghasia zilizoshika kasi
wakaazi wanaishi karibu na msikiti mwekundu wakimbia ghasia zilizoshika kasiPicha: AP

Taarifa zinasema kiasi cha makamanda watatu wa polisi na wapiganaji takriban 40 wameuwawa na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa hivi punde katika mapambano yanayoendelea kwenye msikiti wenye mzozo mjini Islamabad.

Vikosi vya wanajeshi katika mji wa Islamabad walianzisha mapema hii leo opresheni ya kuuvamia msikiti mwekundu baada ya kuvunjika mazungumzo ya kutafuta suluhu na viongozi wenye itikadi kali katika msikiti huo.

Tayari inaarifiwa wanajeshi wameingia ndani ya ua wa msikiti huo .

Miripuko mikubwa na mashambuliano ya risasi yamesikika kwenye eneo hilo.

Msemaji wa jeshi Major Generali Waheed Arshad amesema palikuwepo matumaini ya kupatikana ufumbuzi juu ya mzozo huu lakini ujumbe wa serikali uliokwenda kujaribu kufikia makubaliano na viongozi wa msikiti huo wamejiondoa kwenye mazungumzo hayo mapema hii leo.

Mawaziri nchini Pakistan wanamshutumu kiongozi wa msikiti lal Masjid mwenye msimamo mkali pamoja na wafuasi wake kwa kuwatumia wanawake na watoto kama ngao ya kinga.