1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SIPRI: Matumizi ya kijeshi duniani yaliongezeka 2023

Lilian Mtono
22 Aprili 2024

Ripoti ya taasisi ya utafiti wa masuala ya amani ya Stockholm, SIPRI, imebaini ongezeko la matumizi ya kijeshi kote ulimwenguni kwa asilimia 7 ambayo ni sawa na dola bilioni 2,433 kwa mwaka 2023.

https://p.dw.com/p/4f2am
Marekani| Kifaru
Zana za kijeshi za MarekaniPicha: Andreea Alexandru/AP/dpa/picture alliance

Ripoti ya taasisi ya utafiti wa masuala ya amani ya Stockholm, SIPRI, imebaini ongezeko la matumizi ya kijeshi kote ulimwenguni kwa asilimia 7 ambayo ni sawa na dola bilioni 2,433 kwa mwaka 2023.

Ongezeko hilo kulingana na SIPRI ni la juu kabisa kwa mwaka tangu mwaka 2009.

Taasisi hiyo imesema kwenye taarifa yake kwamba mataifa 10 yaliyokuwa na matumizi makubwa kabisa ya kijeshi kwa mwaka huo wa 2023 yaliongozwa na Marekani, China na Urusi, ambayo kwa pamoja yaliongeza matumizi yao ya kijeshi.

Mtafiti mwandamizi wa Programu ya Matumizi ya Kijeshi na Uzalishaji wa Silaha kwenye taasisi hiyo, Nan Tian, amesema ongezeko hilo linahusiana moja kwa moja na namna mataifa yalivyotumia nguvu za kijeshi kushughulikia mizozo ulimwenguni.