1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Somalia yamfukuza balozi wa Ethiopia na kufunga ubalozi

5 Aprili 2024

Somalia imemfukuza balozi wa Ethiopia, kuzifunga balozi mbili ndogo za Ethiopia nchini humo pamoja na kumuita nyumbani balozi wake aliyeko nchini Ethiopia katikati ya mzozo baina ya mataifa hayo ya pembe ya Afrika

https://p.dw.com/p/4eSdw
Rais| Somalia / Hassan Sheikh Mohamud
Rais wa Somalia Hassan Sheikh MohamudPicha: REUTERS

Somalia imemfukuza Balozi wa Ethiopia, kuzifunga balozi mbili ndogo za Ethiopia nchini humo pamoja na kumuita nyumbani balozi wake aliyeko nchini Ethiopia katikati ya mzozo baina ya mataifa hayo jirani kuhusiana na mpango wa Ethiopia wa kujenga kambi ya kijeshi katika jimbo lililojitenga la Somaliland.

Taarifa ya Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ethiopia Nebiyu Tedla amesema nchi yake haikuwa na taarifa kuhusu suala hilo ambalo lilitangazwa rasmi na ofisi ya Waziri Mkuu wa Somalia.

Soma zaidi. Somalia yamfukuza balozi wa Ethiopia

Wizara ya Mambo ya Nje ya Somalia imesema imefikia uamuzi huo kutokana na vitendo vya serikali Shirikisho ya Ethiopia ambavyo imevitaja kuwa vinakiuka uhuru wa Somalia na mambo ya ndani ya nchi hiyo.

Wizara hiyo ya mambo ya nje ya imeeleza pia katika taarifa yake kwamba imempa balozi wa Ethiopia saa 72 kuondoka nchini humo na kuamuru kufungwa kwa ofisi za ubalozi wa Ethiopia katika eneo lilojitenga la Somaliland na Putland.

Maafisa wa Somaliland: Amri hiyo haitekelezeki.

Maafisa wakuu kutoka maeneo ya Somaliland na Puntland ambayo yamo kwenye mzozo wa kikatiba na Mogadishu wamesema amri hiyo ya Wizara ya Mambo ya nje ya Somalia haiwezi kutekelezwa katika maeneo yao.

Somalia/ Ethiopia
Maelfu ya waandamanaji mjini Mogadishu wakiandamana kufuatia Somaliland kuingia makubaliano na Ethiopia ya kujenga kambi ya kijeshi kwenye ukanda wa pwani ya SomalilandPicha: Farah Abdi Warsameh/AP/picture alliance

Akijibu amri hiyo, Naibu Waziri wa Mambo ya nje wa Somaliland, Rhoda Elmisaid ametumia mtandao wa kijamii wa X kutuma ujumbe kwa shirika la habari la Reuters akisema kwamba Somaliland ni nchi huru na inayojitegemea.

Kwa upande wake, Mohamud Aydid Dirir, Waziri wa habari wa Puntland,ameiambia redio ya idhaa ya Somalia ya Sauti ya Amerika kuwa uamuzi uliotolewa na Somalia hauwezi kutekelezwa Somaliland na Putland na kwamba hawawezi kuzifunga balozi za Ethiopia katika maeneo hayo.

Soma zaidi. Somalia: Puntland kutotambua taasisi za serikali

Maafisa wawili wa Somalia wamesema hatua hizo zimetokana na mzozo wa mkataba wa makubaliano wa Ethiopia ambayo haina bandari uliosaniwa Januari Mosi wa kukodi kilomita 20 za ukanda wa pwani ya Somaliland, eneo ambalo Somalia inasema kuwa ni himaya yake, ingawa eneo hilo limekuwa na utawala wake wa ndani tangu mwaka 1991.

Ethiopia ilisema inataka kujenga kambi ya jeshi huko na kuahidi uwezekano wa kuitambua Somaliland kwa mabadilishano, hatua iliyoighadhabisha Somalia na kuibua hofu mkataba huo ungeliyumbisha zaidi eneo la Pembe ya Afrika.

| Somalia / Rais/  Hassan Sheikh Mohamud
Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud alitoa wito hapo awali kuwa mkataba wa bandari ni kinyume cha sheria na akasema mwezi Februari kuwa nchi yake itajchukuwa hatua zaidi ikiwa Ethiopia itaendelea na mpango huoPicha: REUTERS

Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud alitoa wito hapo awali kuwa mkataba wa bandari ni kinyume cha sheria na akasema mwezi Februari kuwa nchi yake itajchukuwa hatua zaidi ikiwa Ethiopia itaendelea na mpango huo.

Soma zaidi. HRW yaitaka Somalia kutobadili sheria ya haki za watoto

Hata hivyo, Mvutano kati ya Mogadishu na Puntland uliongezeka zaidi mwishoni mwa wiki iliyopita wakati baraza la jimbo la Puntland liliposema kuwa limejiondoa kwenye mfumo wa shirikisho wa nchi hiyo na kwamba watajitegemea kufanya mabadiliko ya kikatiba.

Hatua ya Somalia kumfukuza balozi wa Ethiopia na kufunga balozi zingine ndogo kunaibua wasiwasi juu ya hatma ya wanajeshi 3000 wa Ethiopia walioko Somalia kama sehemu ya kikosi cha walinda amani wa Umoja wa Afrika wanaopmabana na  kundi la wanamgamboi wa Al Shabaab.