1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Steinmeier ahimiza hatua kali dhidi ya Boko Haram

27 Oktoba 2014

Ujerumani imedhamiria kuwashughulikia zaidi wahanga wa mashambulio ya Boko Haram.Amesema hayo waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier akiwa zirani Nigeria.

https://p.dw.com/p/1Dcpb
Waziri wa Mambo ya nchi za nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier (kulia) na waziri mwenzake wa Ufaransa Laurent Fabius bada ya mazungumzo pamoja na wawakilishi wa mashirika ya jamii mjini AbujaPicha: picture-alliance/dpa/Bernd von Jutrczenka

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier na mwenzake wa Ufaransa Laurent Fabius kwa pamoja waliitembelea Nigeria hii leo.Wakati wa ziara yao hiyo fupi mjini Abuja,wanasiasa hao wawili walikutana pia na rais Goodluck Jonathan wa Nigeria pamoja na mawaziri kadhaa na kuzungumzia masuala ya kisiasa na kiuchumi.

Akizungumza na waandishi habari waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani ameshadidia utayarifu wa Ujerumani kuisaidia Nigeria katika juhudi zake za kupambana na wanamgambo wa Boko Haram.Waziri Steinmeier anasema:"Tutazungumza na serikali ya Nigeria kama misada inahitahitajika,mfano katika kuwasaidia polisi na katika shughuli za usimamizi wa maeneo ya mpakani.Yadhihirika kana kwamba wanamgambo wa Boko Haram wanarejea Nigeria baada ya kufanya mashambulio yao katika nchi jirani.Kuwapatia mafunzo polisi pia ni muhimu.Sawa na kupatiwa haraka misaada wahanga wa vituko vya Boko Haram.Upande huo pia Ujerumani na Ufaransa zinaweza kushirikina."

Steinmeier ahimiza pia rushwa ikome

Mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani na Ufaransa Frank-Walter Steinmeier na Laurent Fabius walikutana pia na wawakilishi wa mashirika ya jamii.

Frank-Walter Steinmeier in Nigeria 27.10.
Waziri Steinmeier (Kati),waziri mwenzake wa Ufaransa Fabius (wa pili kushoto) na wawakilishi wa mashirika ya jamii akiwemo Florence Ozor (watatu kutoka kushoto)Picha: picture-alliance/dpa/Bernd von Jutrczenka

Mashirika ya jamii nchini Ujerumani yanamtaka waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani Steinmeier atilie mkazo pia umuhimu wa kupambana na rushwa na kulaani ufisadi ,mambo yanayoangaliwa kama chazo cha matumizi ya nguvu nchini Nigeria.Hii ni mara ya kwanza kwa mawaziri hawa wawili kufanya ziara ya pamoja katika eneo la Afrika kusini mwa bara la sahara.Ziara hii ya pamoja ni kitambulisho cha ushirikiano kati ya Ujerumani na Ufaransa na pia ishra ya juhudi za pamoja katika kukabiliana na mizozo ya kimataifa.

Mwandishi:Kriesch Andrian/Scholz,Jan-Philipp

Tafsiri:Hamidou Oummilkheir

Mhariri:Yusuf Saumu