1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Steinmeier-Togo

12 Februari 2008

Waziri wa nje wa Ujerumani amewasili leo Burkina Faso baada ya ziara yake jana nchini Togo-koloni la zamani la Ujerumani.

https://p.dw.com/p/D6HB

Waziri wa nje wa Ujerumani Walter Steinmeier,akiendelea na ziara yake ya Afrika magharibi amewasili Burkina Faso akitokea nchini Togo koloni la zamani la mjeru mani mpaka viliporipuka vita vya kwanza vya dunia.Mahusiano baina ya Togo na Ujerumani hadi leo ni makubwa.Katika medani ya kisiasa hakuna mengi yaliopita kati ya pande hizi mbili katika kipindi kilichopita.Wakati kwahivyo, ukawadia jana kwa waziri wa nje wa Ujerumani kufanya ziara ya kwanza ya mjumbe wa serikali ya Ujerumani nchini Togo.

Ukumbi wa waandishi habari wa wizara ya nje ya Togo ulisheheni ukiwasubiri mawaziri wa nje wa Ujerumani na wa Togo.Miongoni mwa waandishi habari waliokua wakisubiri kwa hamu kuu ni John Zodzi.Anasema:

"Kwani imepita miaka 15 hadi sasa mjumbe wa serikali ya Ujerumani kuwasili hapa kwetu.hii ilitokana na machafuko hapa nchini Togo.Serikali ya ujerumani ilisimamisha ushirikiano wake na Togo na ikidai bila kigeugeu demokrasia."

Tangu kufanyika uchaguzi wa Bunge hapo oktoba mwaka jana ambamo Upinzani uliruhusiwa kushiriki hali ya kisiasa nchini Togo imeanza kupambazuka.Kufuatia kufariki kwa rais Eyadema ,alietawala kipindi kirefu tena kwa mabavu hapo 2005,machafuko ya umwagaji damu yalitokea ambayo waziri wa nje wa ujerumani Bw.Steinmeier jana alikumbusha:

"Togo imejionea miaka 2 ya maovu makubwa.Miaka ambayo sio tu iligubikwa na misiba ya kimaumbile,lakini hasa na balaa la kisiasa la kukandamizwa kwa upinzani na kuongoza machafuko mitaani.Umma nchini humu sasa umeikomboa kidogo demokrasia.Kupitia uchaguzi wa Oktoba mwaka uliopita sasa tunanyosha njia bora.Sisi wajerumani na jamii ya kimataifa tuna nafasi sasa kuungamkono mkondo huu."

Mwaka 2005 mtoto wa jamadari Eyadema Faure Gnassingbe aliamua kukalia kiti cha baba yake na kupitia uchaguzi wa mizengwe alipanga kujithibitisha madarakani.Wafuasi wa upinzani waliochoshwa na utawala wa baba yake wakaandamana na vikosi vya usalama vikawafyatulia risasi na mamia wakauwawa.Maalfu ya watogo wakaikimbia nchi yao.Gnassingbe hatahivyo, alin'gan'gania madaraka .Alitangaza lakini yutayari kwa sera za mageuzi nchini Togo na juu ya mageuzi hayo alizungumza na mgeni wake waziri wa nje wa Ujerumani hapo jana:

Bw.steinmeier alisema:

"Miongoni mwa mageuzi hayo ni mfumo wa vyombo vya usalama na hii ni sawa kabisa ikiwa pawepo mtengano wazi wa mamlaka kati ya kikosi cha polisi na jeshi."

Togo iko mbali mno kuitwa dola linaloegemea sheria,kwani serikali haiguswi inapokanyaga haki na sheria na kwa maafa yaliotokea katika machafuko ya 2005 hakuna yeyote aliehukumiwa .Waziri wa nje wa Ujerumani kwahivyo, alimzindua mwenyeji wake kuhimiza suluhu na maskizano nchini togo.Lamkini hata Togo nayo imeelezea matarajio yake kutoka Ujerumani ambayo yanatokana kwa ajili au licha ya miaka 30 ya ukoloni wa Ujerumani nchini Togo.Kwa muujibu wa waziri wa nje wa Togo,nchi yake inatazamia ushirikiano zaidi na msaada zaidi kutoka Berlin.