1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

STRAßBOURG:Angela Merkel aahidi kuanzisha majadiliano ya katiba ya Ulaya

17 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCZx

Kansela wa Ujerumani Bi Angela Merkel anahutubia Bunge la Umoja wa Ulaya mjini Straßbourg nchini Ufaransa ili kuelezea ajenda ya nchi yake inapoanza kutekeleza majukumu yake kama kiongozi wa Umoja wa Ulaya kwa miezi sita ijayo.Nchi ya Ujerumani ilishika hatamu za uongozi wa Umoja huo Januari Mosi mwaka huu.Bi Merkel anatarajiwa kupigia debe juhudi zake za kujadilia tena katiba ya Umoja wa Ulaya iliyokataliwa na wapiga kura kutoka mataifa ya Ufaransa na Uholanzi mwaka juzi.Malengo mengine ya kiongozi huyo ni kujaribu kuafikiana kuhusu sera ya pamoja ya nishati ili kuhakikisha kuwa uzalishaji unaimarishwa vilevile ushirikiano katika sera za kigeni katika mataifa wanachama wa Umoja wa Ulaya.