1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sudan kusini yatakiwa kuheshimu haki za wa wanawake

14 Juni 2013

Miongoni mwa matatizo ya kijamii yanayolikabili taiafa changa la Sudan kusini, kubwa ni mtindo wa watoto wadogo kuolewa mapema. Licha ya kuwepo sheria za kuwalinda lakini sheria hizo bado hazifanyi kazi ipasavyo.

https://p.dw.com/p/18q3s
Rais wa Sudana Kusini Salva Kiir Mayardit
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir MayarditPicha: picture alliance / ZUMA Press

Akech B alipenda sana kusoma akiwa na ndoto za kuwa muuguzi siku moja. Lakini wakati alipokuwa na miaka14, mjomba wake ambaye alikuwa akimsaidia alimlazimisha kuacha shule ili akaolewe na mwanaume.

Akech anasema mwanaume huyo alikuwa mtu mzima mwenye mvi, ambaye alilipa ng'ombe 75 kama mahari ya Akech kuolewana mwanaume ambaye alishaoa na kupata watoto kadhaa. Akech alijaribu kupinga ndoa hiyo, lakini mjomba wake aliendelea kusisitiza “ wasichana wamezaliwa kwa ajili ya kutumiwa na wanaume'' yote hayo ni kwa lengo la kupata mahari yake.

Licha ya binamu zake kumpiga na kumpeleka nyumbani kwa mwanaume huyo, lakini Akech mara zote amekuwa akijificha kwa marafiki zake. Lakini mjomba wake anamtafuta na kumpeleka jela akiwambia maofisa wa jila, Akech anamkimbia mume wake na inatahitajika kupewa somo.Baada ya hapo Akech akaona hakuna jinsi ila kuishi.

Habari kama hizi za Akech zimewakuta wanawake wengi waliofanyiwa mahojiano kati ya kipindi cha mwezi Machi na Oktoba mwaka 2012 nchini Sudan Kusini ambapo tabia ya kuwaoza watoto wadogo ni janga kwa wasichana nchini humo.

Ndoa za watoto wadogo bado ni tatizo sudan Kusini

Zaidi ya nusu ya wasichana wenye umri wa kati ya miaka 15 na 19 nchini Sudan Kusini wanaolewa mapema, ikiwa ni kwa mujibu wa utafiti wa serikakali ya nchi hiyo. Wasichana ambao wanajaribu kupinga ndoa za lazima wanakabiliwa na mateso makubwa kutoka familia zao.

Akinamama Sudan Kusini
Akinamama Sudan KusiniPicha: Getty Images

Katika kadhia ambazo zilifuatiliwa na shirika la kuetetea haki za binadamu Ulimwenguni Human Rights Watch inaonesha wasischana wanapigwa, kutolewa maneno machafu na kutishiwa kuwa wao ni mkosi au kupelekwa poilisi ili kuwalazimisha kuolewa.

Wakati mwengine hufungwa au kuuawa na familia zao. Jamii za watu wa Sudan Kusini wanaona utamaduni wa kuwaoza watoto wadogo kama jamabo la kufurahisha wasichana wao na familia zao.

Inaonekana njia muhimu kwa familia hizo kujipatia utajiri kupitia vitendo hivyo vya kitamaduni vya kuhamisha utajiri wa wanyama, pesa na zawadi zingine kupitia malipo ya mahari. Lakini uhalisia ni tofauti na ilivyo,kwani wasichana hao wanaachishwa shule wakinyimwa haki ya kupata elimu.

Utafiti wa kiafya unaonesha wasichana waliolewa wakiwa wadogo, wanakabiliwa na hatari kubwa wakati wa ujauzito na kujifungua, kulikoni waliolewa wakubwa. Seriakali ya Sudan Kusini tayari imechukua hatua kadhaa kupambana na ndoa hizo, kwa kuweka sheria za ambazo zinatoa umuhimu katika kulinda kuwaoza watoto na wanawake katika ndoa zao.

Kuna juhudi pia ya kuendeleza mpango wa wasichana kupata elimu hata kwa kutumia njia mbadala za kupata elimu ambayo inawawezesha wasichana, wakinamama na watu wengine waliopata ujauzito na hawakuwa na njia ya kuendelea na masomo, au wale ambao wamekatishwa masomo yao.

Sheria ya kupinga ndoa za watoto wadogo haipewi umuhimu

Kuna tabaka na na hali ya kutokueleweka sheria iliowekwa kulinda haki za akina mama na wasichana lakini sheria hizo zinakabiliwa na kutokuwa na mshikamano hasa kwa mawaziri mbao ndiyo wanye majukumu ya kupambana na ndoa hizo.

Rais wa Sudan Kusini na viongozi kadhaa
Rais wa Sudan Kusini na viongozi kadhaaPicha: Jenny Vaughan/AFP/Getty Images

Matokeo ya kushindwa huko, wanawake wengi na wasichana wanandelea kupata tabu na kuishi katika mazingira ambayo yanaedeleza mpango wa kuwaoza wsicchana wadogo. Wakati ambapo Juni 16 serikali ya Sudan kusini na nchi nyingine za bara la Afrika zitadhimisha siku ya mtoto wa Afrika, serikali ya Sudan Kusini inatakiwa kuchukua hatua ya muda mrefu ya kuzuia wasichana kufanyiwa vitendo hivyo vichafu, na kuhakikisha haki zao zinaheshimiwa.

Ni muhimu kwa seriakli ya Sudan kusini kuchukua hatua hiyo kwani, ndoa hizo zinakwamisha maendeleo ya kijamii, kielimu, kiuchumi, kiafya na usalama wa wanawake na wasichana wadogo katika familia na jamii zao. Kushindwa kupambana na ndoa hizo, kunaonekana kukwamisha utekelezaji wa juhudi za kuleta maendeleo ya baadaye kwa sudan Kusini.

Mwandishi: Hashimu GUlana/IPS

Mhariri:Abdul-Rahman