1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sudan yaadhimisha mwaka mmoja wa mapinduzi dhidi ya Bashir

Sekione Kitojo
11 Aprili 2020

Ni mwaka wa kwanza wa Sudan tangu kuondolewa kwa dikteta Omar al-Bashir. Lakini hakuna cha  kusherehekea. Uchumi bado uko dhaifu, hali ya kisiasa bado ni tete, wakati janga  la COVID-19 linazusha mtafaruku mwingine.

https://p.dw.com/p/3alsp
BG Frauen im Sudan
Picha: Getty Images/AFP

Mwaka mmoja  uliopita , mamia  kwa  maelfu ya  raia  wa  Sudan  walifanya maandamano  ya wiki  nzima mbele ya  makao makuu  ya  jeshi  katika  mji mkuu  wa  nchi  hiyo  Khartoum.

Sudan, politische Unruhe
Kiongozi wa maandamano nchini Sudan Ahmed Rabie akionesha ishara ya ushindi pamoja na jenerali wa jeshi Abdel Fattah al-BurhanPicha: Getty Images/E. Hamid

Mwanafunzi kijana  mwanamke , Alla Salah , alisimama  juu  ya  kipaa  cha  gari  akiimba kauli mbiu za kisiasa, baadaye  alikuja  kuwa  ishara  ya  vuguvugu la maandamano  katika jamii  ambayo  kwa  kiasi  kikubwa  inadhibitiwa  na  wanaume zaidi.

Kila  mmoja  aliingia  mitaani, ikiwa  ni  pamoja  na  maprofesa, waalimu  na  madaktari. Wasanii waliandika  ujumbe  na kuchora   picha za  uhuru katika  kuta mjini  Khartoum.

Kwa miezi  kadhaa , nchi  hiyo  ilikuwa  ikitokota  hadi  hatimaye  kile  ambacho hakikufikirika  kikatokea: dikteta  Omar al-Bashir alipinduliwa  Aprili 11, 2019, baada  ya karibu miongo mitatu  madarakani.

Yalikuwa  mapinduzi  yaliyoelezwa  na  wengi  kuwa  ni vuguvugu  la  mapinduzi ya  mataifa ya  Kiarabu namba  mbili. Raia walijisikia  furaha  kubwa.

Sudan, politische Unruhe
Vijana wa Sudan walijiunga na maandamano Picha: AFP/E. Hamid

Lakini  mwaka  mmoja  baadaye, katika  kusherehekea  mwaka  mmoja  wa siku hii  kubwa, hali mjini  Khartoum imenyong'onyea.

Kwasababu  ya  janga  la  virusi  vya  corona, shule  na  vyuo  vikuu vimefungwa. Sherehe  za maadhimisho , kupeperusha  bendera na kuimba wimbo  wa  taifa  ama  nyimbo  za mapinduzi, vimefanyika  nyumbani  ama  katika   mitandao  ya  kijamii.

Lakini  kuna  sababu  nyingine  ya hali  hiyo ya  kunyong'onyea: Baada  ya  miezi 12 ya  uhuru wa  kisiasa , Sudan  haijapiga  hatua  ambayo ilipigiwa  matumaini.

BG Frauen im Sudan
Mwanamke Alla Salah aliyepata umaarufu katika maandamano ya kumuondoa dikteta Omar al-Bashir nchini SudanPicha: Getty Images/AFP

Nchi  hiyo  iko imara kisiasa  lakini  tete. Uchumi  wake  umeporomoka kabisa, na  janga  la virusi  vya  corona , linatishia  kuharibu  mafanikio  madogo  nchi  hiyo  iliyoyapata  katika miezi 12 iliyopita  katika  kufufua  biashara  na  uchumi.

Sudan ni mshirika  mdau muhimu  katika  eneo  la kanda hiyo. Ni nchi  ya  tatu  kwa  mkubwa katika  bara  la  Afrika , pamoja  na  watu  wake  milioni  42 inaonekana  kuwa  ni  daraja  kati ya  Afrika  na  ulimwengu  wa  Kiarabu. Sudan  pia  ni  moja kati  ya  nchi  muhimu za  kupitia watu  wanaokwenda  kusaka  uhamiaji  kutoka  bara  la  Afrika.

Iwapo  hali  ya  kisiasa  na  kiuchumi  itakuwa  bora , Sudan  inaweza  kutoa  fursa  ya uwekezaji  kutoka  nje, kwa  mfano  katika  sekta  ya  mafuta  na  kilimo.

Sudan Khartum | Ex-Präsident Umar al-Baschir vor Gericht
Omar al-Bashir hatimaye akiwa mfungwa Picha: Getty Images/AFP/E. Hamid

Lakini  kwa  hivi  sasa , Sudan  imelala, na  kutishia  kuleta  madhara  makubwa  kutokana  na hali  hiyo kwa eneo  la  kanda  hiyo, anasema  Philipp Jahn , mkuu wa  kituo cha  utafiti  wa wakfu  wa Friedrich Ebert  nchini  Sudan.

Licha  ya  mabadiliko  chanya  ya  kisiasa , Sudan  haikuweza