1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SYDNEY : China katika nadhari ya mkutano wa APEC

6 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBSN

China leo inawekewa nadhari kuu katika mkutano wa viongozi wa Asia na Pasifiki wakati Rais Hu Jintao wa China anapokutana na Rais George W. Bush wa Marekani na Waziri Mkuu wa Australia John Howard katika mazungumzo juu ya usalama,usalama wa bidhaa na mabadiliko ya hali ya hewa.

Howard alirasimu Azimio la Sydney juu ya mabadiliko ya hali ya hewa ambalo inaonekana limefanyiwa mabadiliko fulani baada ya rasimu yake ya awali kuvujishwa na makundi ya wanaharakati mwezi uliopita.

Rasimu hiyo inatowa wito wa kuwepo kwa malengo ya kutaka kufikiwa kwa ufanisi wa nishati badala ya kuweka malengo ya kushurutisha na kuhamisha teknolojia ya utowaji wa gesi chafu ili kuzisaidia nchi zinazoinukia kiuchumi za APEC kuendana na hali ya mabadiliko ya hali ya hewa duniani.