1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SYDNEY:Kisanduku cheusi cha ndege iliyodondoka chapatikana

7 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCLN

Wachunguzi nchini Indonesia wamepata kisanduku cheusi cha maelezo ya safari za ndege kilichokuwa kwenye ndege iliyodondoka kisiwani Java.Chanzo cha ajali hiyo bado hakijulikani japo kwa mujibu wa Waziri Mkuu wa Australia John Howard hakuna chochote kinachoonyesha kuwa ajali hiyo ilisababishwa na vitendo vya ugaidi.Ndege hiyo ya kampuni ya Garuda ilidondoka na kulazimika kutua kwa dharura kwenye uwanja wa ndege wa Yogyakarta kisiwani Java.Baaada ya kutua iliteketekea pale moto ulipofika kwenye tangi la mafuta.

Kwa mujibu wa Waziri Mkuu wa Australia John Howard raia 10 wa nchi yake walikuwa safarini katika ndege hiyo.Baadhi yao ni waandishi 10 wa Australia walioambatana na maafisa wa serikali waliokuwa kwenye ndege hiyo wakielekea nchini Indonesia kwa ziara rasmi.Mawaziri husika hawakuwako katika ndege hiyo.

Picha za video zilizonaswa na mpiga picha wa Kituo cha Seven cha televisheni cha Australia aliyenusurika,zinaonyesha namna abiria hao waliolowa damu walivyotia juhudi kukimbia.Mlipuko mkubwa ulitokea pale moto ulipofika katika tangi la mafuta na kuteketeza baadhi ya abiria waliokuwa wamelala chini.

Rais Susilo Bambang Yudhoyono wa Indonesia ameagiza uchunguzi wa kina kufanyika na kumteua Waziri wa Usalama kujua chanzo cha ajali hiyo ikiwemo uwezekano wa sababu zisizo za kiufundi.Hii ni ajali ya pili mbaya ya ndege nchini Indonesia kutokea mwaka huu.