1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SYDNEY:Madaktari wahojiwa na polisi

6 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBlL

Polisi nchini Australia wamewahoji madaktari wengine watano na kufanya msako katika hospitali mbili ili kutafuta watu wanaoaminika kuhusika na jaribio la shambulio la wiki jana nchini Uingereza.Hatua hiyo inachukuliwa baada ya daktari mmoja aliye na asili ya Kihindi kukamatwa mwanzoni mwa wiki hii katika jimbo la mashariki la Queensland.Yapata madaktari wengine 5 walizuiliwa nchini Uingereza kuhusiana na jaribio hilo la shambulio la bomu katika miji ya Glasgow na London.

Polisi walisaka miji ya Perth na Kalgoorlie magharibi mwa Australia na kuwahoji kwa muda mfupi madaktari 4 walio na asili ya Kihindi waliofanyakazi awali nchini Uingereza.

Misako hiyo na mahojiano inatokea siku moja baada ya maafisa wa huduma za afya katika eneo la magharibi mwa Australia kudai kwamba madaktari wawili wanaozuiliwa na polisi wa Uingereza walijaribu kutafuta kazi nchini Australia bila kufanikiwa.Madaktari hao walizuiliwa kuhusiana na jaribio la shambulio la bomu nchini Uingereza.