1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Syria iache kutumia mabavu dhidi ya waandamanaji

5 Mei 2011

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amemtaka Rais wa Syria Bashar al-Assad kukomesha umwagaji damu na kuwakamata kiholela, wapinzani wanaoandamana kwa amani.

https://p.dw.com/p/RM6p
(110209) -- NEW YORK, Feb. 9, 2011 () -- UN Secretary-General Ban Ki-moon speaks to media during a press conference at the UN headquarters in New York, the United States, Feb. 8, 2011. Ban Ki-moon on Tuesday called for "an orderly and peaceful transition" in Egypt and voiced his hope that "genuine dialogue between the leaders and the people will lead to the beginning of such a process." (/Shen Hong)(axy)
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moonPicha: Picture Alliance/Photoshot

Katibu Mkuu, Ban Ki-moon, ni miongoni mwa viongozi wachache wa kimataifa, kuweza kuzungumza binafsi na Assad kwa njia ya simu, tangu maandamano ya upinzani kuibuka nchini Syria katikati ya mwezi wa Machi. Ban Ki-moon amesema kuwa mageuzi yaliyoahidiwa kufanywa na serikali ya Rais Bashar al-Assad yanapaswa kutekelezwa mapema na kwa ukamilifu. Amesisitiza umuhimu wa kushiriki katika majadiliano yalio wazi na kweli, yakizingatia mchakato wa mageuzi. Rais al-Assad vile vile ashirikiane na tume ya Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kuchunguza machafuko ya nchini humo.

Syria itazidi kutengwa

U.S. Secretary of State Hillary Rodham Clinton, left, and Italian Foreign Minister Franco Frattini, during a press conference ahead of a diplomatic meeting on Libya at Rome's Foreign Ministry, Thursday, May 5, 2011. U.S. Secretary of State Hillary Rodham Clinton says ousting Libyan leader Moammar Gadhafi from his four-decade grip on power is the best way to protect civilians. The meeting of the Libyan Contact Group at the Italian Foreign Ministry on Thursday is expected to seek ways to give financial support to the rebels. (AP Photo/Pier Paolo Cito)
Waziri wa Nje wa marekani Hillary Clinton na waziri mwenzake wa Italia Franco FrattiniPicha: AP

Wakati huo huo, Marekani na Italia zimeionya Syria kuwa itakabiliwa na vikwazo vingine na itazidi kutengwa, ikiwa haitoacha kutumia mabavu dhidi ya waandamanaji wanaodai mageuzi nchini humo. Leo, katika mkutano na waandishi wa habari mjini Rome, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton na waziri mwenzake wa Italia, Franco Frattini walisema kuwa serikali ya Syria yapaswa kushinikizwa kukomesha matumizi ya nguvu yaliyosababisha vifo vya mamia ya watu, tangu maandamano ya upinzani kuanza nchini humo. Ripoti zinasema wanajeshi kadhaa pia waliuawa katika machafuko hayo.

Operesheni ya Daraa yakamilishwa

Kwa mujibu wa makundi ya haki za binadamu, zaidi ya watu 600 wameuawa tangu maandamano hayo ya upinzani kuanza nchini Syria tarehe 15 mwezi Machi. Kundi la haki za binadamu la Syria "Insan" linasema,hadi watu 8,000 wameorodheshwa kama wale waliokamatwa au wasiojulikana walipo. Kwa upande mwingine, hii leo televisheni ya taifa ya Syria imesema kuwa wanajeshi wameanza kuondoka katika mji wa kusini wa Daraa, kitovu cha upinzani dhidi ya serikali. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, wanajeshi wameshakamilisha operesheni yao kwa kuwakamata wale walioitwa "magaidi" na kwamba wamefanikiwa kurejesha utulivu.

Wanajeshi watumiwa kuzima upinzani

epa02706758 A TV handout grab taken from Al Arabiya channel on 28 April 2011, shows a Syrian tank and soldiers moving in the city of Daraa, Syria. According to media sources, the Syrian army was said to be deploying tanks on 26 April in its advance towards several cities, as international condemnation of the government's use of violence against peaceful protesters grew. Witnesses said tanks and sharp shooters were seen throughout Daraa. EPA/AL ARABIYA / HANDOUT BEST QUALITY AVAILABLE. EPA IS USING AN IMAGE FROM AN ALTERNATIVE SOURCE, THEREFORE EPA COULD NOT CONFIRM THE EXACT DATE AND SOURCE OF THE IMAGE, HANDOUT EDITORIAL USE ONLY/NO SALES +++(c) dpa - Bildfunk+++
Vifaru vya Syria vilivyotumiwa kukandamiza upinzani mji wa DaraaPicha: picture alliance / dpa

Wakati huo huo, mwanaharakati mmoja nchini Syria, ameripoti kuwa zaidi ya watu 300 wamekamatwa katika mji wa Saqba ulio nje ya mji mkuu Damascus, wakati vikosi vya usalama, vikiendelea kutumia nguvu katika jitahada ya kukandamiza upinzani nchini humo. Mwanaharakati huyo ambae hakutaka kutajwa kwa jina, ameliambia shirika la habari la AFP kuwa vikosi vya usalama vilisaidiwa na wanajeshi. Afisa mmoja wa Kiarabu anaefuatiliza matukio ya nchini Syria, anasema, uamuzi wa Assad kutumia majeshi ni ishara kuwa kiongozi huyo hataki maridhiano.

Mwandishi: Martin,Prema/RTRE/AFPE

Mhariri:Josephat Charo