1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Taasisi ya Goethe yafunguliwa rasmi jijini Dar es Salaam

Josephat Nyiro Charo8 Aprili 2010

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani, Guido Westerwelle, na mwenzake wa misaada ya maendeleo, Dirk Niebel, wamemaliza ziara yao nchini Tanzania kwa waziri Westerwelle kuizindua taasisi ya Goethe

https://p.dw.com/p/MrCi
Taasisi ya Goethe- jijini Dar es Salaam, TansaniaPicha: DW

Taasisi ya Utamaduni wa Kijerumani ya Goethe pamoja na mambo mengine, hutoa pia mafunzo ya lugha ya Kijerumani.

Ujerumani na Tanzania zimekuwa na ushirikiano wa karibu kwa muda mrefu, hivyo kuzinduliwa kwa kituo hicho kunaimarisha mahusiano ya karibu baina ya wananchi wa nchi hizo mbili. Kutoka Dar es Salaam mwandishi wetu George Njogopa ametutumia taarifa ifuatayo.

Mtayarishaji: Halima Nyanza

Mhariri: Othman Miraji