1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiUjerumani

Pato la taifa Ujerumani kunywea hadi asilimia 0.5 mwaka 2023

29 Agosti 2023

Taasisi ya uchumi ya Ujerumani imeeleza kuwa nchi hiyo yenye uchumi mkubwa zaidi barani Ulaya inatarajiwa kupungua kwa pato lake jumla la taifa kwa hadi asilimia 0.5 kwa mwaka 2023.

https://p.dw.com/p/4VgIg
Sarafu za Euro hutumiwa na nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya ikiwemo Ujerumani
Sarafu za Euro hutumiwa na nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya ikiwemo UjerumaniPicha: Petr Svancara/CTK Photo/IMAGO

Hali hiyo imetokana na viwango vya juu vya riba, bei za nishati zilizoongezeka na mauzo duni ya bidhaa za nje.

Katika ripoti yake mpya, taasisi hiyo imesema uchumi wa Ujerumani umeathirika hasa kutokana na siasa za kikanda kama vile mzozo wa Ukraine na mivutano yake na China.

Taasisi hiyo ya uchumi inatabiri kuwa, pato jumla la Ujerumani mwishoni mwa mwaka huu 2023 litakuwa sawa kama ilivyokuwa mwaka 2019. Kwa wastani, taasisi hiyo ya IW inataraji kuwepo na watu milioni 2.58 wasiokuwa na ajira mwaka huu 2023, idadi hiyo ikiwa watu 160,000 zaidi ya mwaka uliopita.

Hali hiyo itasababisha kiwango cha ukosefu wa ajira kuongezeka hadi asilimia 5.5.

Kwa ujumla, kiwango cha mfumuko wa bei mwaka 2023 kitakuwa chini kidogo ya kiwango cha mwaka uliopita kwa asilimia 6.5.