1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Taleban washambulia makao mkuu ya Polisi Afghanistan

15 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Cc2u

KABUL.Watu watano wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya gari lililokuwa na milipuko kulipuka nje ya ofisi ya Meya wa jiji la Kabul ambayo inapakana na makao makuu ya polisi.

Kundi la Taliban limedai kuhusika na shambulizi hilo, ambapo limesema kuwa makao makuu hayo ya polisi ndiyo yalikuwa lengo la shambulizi hilo.

Msemaji wa kundi hilo la Taliban Zabiullah Mujahed amesema kuwa shambulizi hilo halikuwa la kujitoa mhanga, mbinu ambazo zimekuwa zikitumiwa na kundi hilo.

Kwa upande wake Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Afghanistan Zemari Bashar amesema kuwa waliyouawa ni raia na kwamba polisi wawili walijeruhiwa.

Tarehe 5 mwezi huu watu 13 waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya mshambuliji wa kitaliban kujitoa mhanga kwa kulibamiza gari lililokuwa na milipuko kwenye basi la jeshi la Afghanistan.