1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TANGAZO MAALUM

15 Februari 2011
https://p.dw.com/p/10HXc
Mtambo wa SatelaitiPicha: AP/ESA

Vipindi vya DW vyalengwa kukorofishwa

Jumatatu tarehe 14.2. 2011 saa saba na dakika saba za mchana kwa saa za UTC, wahandisi wa Deutsche Welle waligundua kukorofishwa kwa matangazo. Mitambo iliyohusika hasa ni ile ya Satelaiti ya Hotbird 8. Kutokana na hali hii matnagazo ya lugha za kigeni yaliingiliwa. Mnamo siku zilizopita yaliingiliwa matangazo kuelekea Iran, mara ya mwisho ikiwa ni Februari 2010.

Ukorofishaji huu umeyagusa matangazo ya DW-TV kwa Ulaya, DW-TV kwa Arabia na frekwensi za FM ma masafa marefu katika maeneo kadhaa ya Ulaya, Mashariki ya Kati na sehemu za Asia. Pia mtandao wa Internet wa Deutsche Welle uliathirika. Mtambo ya Hotbird 8 wenye kutoa huduma kupitia anuani ya DW-WORLD.DE nao pia umekumbwa na athari hiyo.

Idara ya DW inayohusika na usambazaji wa yaliyomo katika matangazo imechukua hatua za marekebisho. Kuhusiana na mtandao wa Internet na urushaji wa matangazo ya Satelaiti pamekodiwa huduma maalum. Redio washirika wa Deutsche Welle wenye kurusha matangazo yake zimearifiwa.

Mwandishi: Birgit Görtz

Mhariri: Marc Koch