1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tanzania: Tundu Lissu mahakamani

Elizabeth Shoo28 Juni 2016

Mwanasiasa huyo wa CHADEMA anashtakiwa na serikali ya Tanzania kwa makosa ikiwemo kula njama ya kutoa chapisho lenye uchochezi akiwa na mwandishi wa habari, mhariri na mchapishaji wa gazeti la Mawio.

https://p.dw.com/p/1JF4y
Tundu Lissu wa CHADEMA
Picha: DW/M.Khelef

[No title]

Kesi ya uchochezi inayomkabili mwanansheria na mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, na wengine watatu akiwemo mhariri na mmiliki wa gazeti la Mawio imeendelea kutajwa katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es salaam, huku ikionekana kuvutia wafuasi wengi wa kisiasa pamoja na wachambuzi wa masuala ya kisisasa.