1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Taylor alichochea vita Sierre-Leone kujitajirisha

8 Januari 2008

---

https://p.dw.com/p/Cljk

THE HAGUE

Shahidi wa kwanza katika kesi ya uhalifu wa kivita dhidi ya kiongozi wa zamani wa Liberia Charles Taylor alitoa ushahidi wake hapo jana akisema madini ya almasi yalikuwa kichocheo kikubwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sierra Leone.Taylor rais wa zamani wa Liberia anatuhumiwa kwa kuamrisha vikosi vya waasi nchini Sierre leone kuua watu kwa kuwakatakata viungo vya mwili.Aidha kiongozi huyo pia anakabiliwa na mashtaka juu ya ubakaji ,mauaji na kuwaingiza watoto jeshini.Pia anashutumiwa kwa kuhusika katika kusababisha machafuko nchini Sierre leone ili ajipatie utajiri wa madini ya almasi ya taifa hilo.Taylor ni kiongozi wa zamani wa kwanza barani Afrika kuwahi kufikishwa mbele ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita.