1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TBILISI: Urusi na Georgia zahimizwa kudumisha utulivu

9 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBaz

Shirika la uhusiano wa kibiashara na maendeleo OECD limeeleza wasiwasi wake juu ya mzozo kati ya Urusi na nchi jirani ya Georgia.

Waziri wa mambo ya nje wa Uhispania Miguel Angel Moratinos ambae ni mwenyekiti wa sasa wa shirika hilo amesema atachunguza madai ya Georgia yanayo ishutumu Urusi kwa kuhusika na shambulio la angani dhidi ya jimbo lililojitenga la Ossetia Kusini.

Georgia imelitaka baraza la usalama la umoja wa mataifa kujadili kitendo cha uchokozi dhidi yake.

Urusi imekanusha madai hayo na kuilaumu Georgia kwa kutekeleza shambulio hilo ili kuzidisha hali ya mivutano katika eneo hilo.

Umoja wa Ulaya na shirika la Uhusiano wa kibiashara na maendeleo zimetowa mwito kwa nchi hizo mbili kuwa na utulivu.