1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TBILISI: Urusi yakosolewa kwa msimamo wake mkali dhidi ya Georgia

21 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD0W

Waziri wa mambo ya kigeni wa Georgia, Gela Bezhuashvili, ameikosoa Urusi kwa msimamo wake mkali dhidi ya Georgia. Aidha kiongozi huyo ameitaka Ulaya isinyamae kimya huku hali ya wasiwasi ikiendelea kuzidi kati ya Georgia na Urusi.

Katika mahojiano yake na shirika la habari la Associated Press leo asubuhi, waziri Gela amemkosoa rais Putin kwa kuwaambia viongozi 25 wa Umoja wa Ulaya mjini Helsinki Finnland, kwamba Georgia inataka kuyachukua tena kwa nguvu maeneo mawili yaliyojitenga nchini Georgia yanayoiunga mkono Urusi.

Rais Putin amesema hatua kali dhidi ya Georgia zinalenga kuzuia malumbano yasiotokee baina ya nchi hizo.