1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tehran. Mjerumani aachiliwa huru baada ya kuhumiwa kifungo.

13 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCJi

Mtalii wa Kijerumani ambaye alitiwa mbaroni pamoja na raia mmoja wa Ufaransa baada ya boti lao kudaiwa kuwa liliingia katika eneo la maji la Iran ameachiwa huru kutoka jela mjini Tehran.

Hii imethibitishwa na waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Frank Walter Steinmeier.

Mtu huyo mwenye umri wa miaka 52 Donald Klein alihukumiwa kwenda jela miezi 18 Januari mwaka jana pamoja na Stephane Lherbier kwa madai ya kuchukua picha za meli katika ghuba ya Persia. Lherbier alisamehewa na kuachiwa huru mwezi uliopita.