1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN: Mripuko mwingine wa bomu nchini Iran

17 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCRK

Ripoti zinasema,mapambano yamezuka kati ya wanamgambo na polisi,kufuatia mripuko wa bomu uliotokea siku ya Ijumaa katika mji wa Zahedan,kusini mashariki mwa Iran.Shirika la habari la serikali IRNA limesema,baada ya mripuko huo,askari polisi walizingira eneo hilo na pande mbili zilifyatuliana risasi.Shambulio hilo limetokea saa chache tu baada ya maziko ya wanajeshi 11 wa Kikosi cha Mapinduzi cha Iran, ambao waliuawa siku ya Jumatatu katika mripuko wa gari.Zaidi ya watu 30 walijeruhiwa katika shambulio hilo.Kundi la Waislamu wa madhehebu ya Sunni liitwalo Jundallah na kufuata siasa kali, limedai kuwa ndio limehusika na shambulio hilo.Mji wa Zahedan unaopakana na Afghanistan na Pakistan una jamii ndogo ya Wabulushi wenye madhehebu ya Sunni.