1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tetemeko la ardhi latikisa sehemu za China

21 Machi 2008
https://p.dw.com/p/DSIq

BEIJING:

Taarifa kutoka China zinaeleza kutokea tetemeko kubwa la ardhi mapema leo katika eneo la Kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo.Hata hivyo hakuna habari za mapema zikionyesha majeruhi.Tetemeko hilo, lililokuwa na nguvu za 7.3 za kipimo cha Ritcher,lilifuatiwa na mitetemeko mingine miwili midogo.Tetemeko hilo limetokea katika eneo ambalo lina idadi ya watu kiasi katika mkoa wa Xinjiang-umbali wa kilomita 230 kusini mashariki mwa mji wa Hotan.