1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tetemeko lauwa watu Pakistan

Kalyango Siraj29 Oktoba 2008

Miili 160 imetolewa na juhudi za uokozi baado zinaendelea

https://p.dw.com/p/FjZR
Mmoja wa waliojeruhiwa katika tetemeko la ardhi PakistanPicha: AP

Takriban watu 160 wanasemekana wamepoteza maisha yao baada ya tetemeko la ardhi kutokea katika vijiji vitatu katika mkoa wa Pakistan wa Baluchistan unaopatikana kusini magharibi mwa nchi hiyo.Maafisa wanasema kuwa idadi hiyo inaweza ikaongezeka.

Tetemeko hilo limetokea jumatano na kituo cha Marekani cha Jiolojia kimepima nguvu za tetemeko hilo na kusema kuwa lilikuwa na nguvu za 6.4 katika vipimo vya Richeter.Mkuu wa kituo cha kutabiri hali ya hewa cha Pakistan mjini Islamabad,Chaudhry anasema na kitovu chake kilikuwa katika umbali wa kilomita 10.

Maafisa wa serikali wanasema kuwa juhudi za kuwaondoa watu kutoka kwa vifusi vya nyumba zilizobomolewa na tetemeko hilo baado zinaendelea. Na miili zaidi ya 160 ilikuwa imetolewa kutoka katika vijiji kadhaa vya Ziarat.

Ziarat ni eneo la bonde ambalo ni kivutio kwa watalii katika mkoa wa Baluchistan, na linapatikana umbali wa kilomita 70 kaskazini mwa Quetta ambao ni mji mkuu wa mkoa huo.

Nyumba kadhaa ziliharibiwa na walioshuhudia wanasema watu walikimbia barabarani wakipiga makelele. Tetemeko hili lilitokea wakati wanavijiji wengi walipokuwa baado wamelala.

Mapema polisi ya wilaya jirani ya Pishin ilisema kuwa watu sita walikuwa wameuawa huko.Tena katika mji wa Sanjawai,mtu mmoja alienusurika ameliambia shirika la habari la AFP kuwa tetemeko la kwanza lilimuamsha kutoka kitandani kabla ya saa kumi na moja alfajiri sa za Pakistan.Baada ya dakika 10 baadae mtu huyo akasikia tetemeko lingine kubwa. Aliongeza kuwa katika Ziarat majengo mengi yalianguka na mawasiliano kukatwa na kuongeza kuwa inaonekana mji huo umeharibiwa vibaya.

Mkuu wa kikosi cha jeshi la Pakistan kilichoko Baluchistan Meja Generali Saleem Nawaz amesema kuwa wahanga wanaaza kusaidiwa.

Yeye msemaji wa jeshi la Pakistan amesema kuwa wanajeshi wapatao 250 wametumwa Ziarat kutoka Quetta pamoja na Helikopta mbili.

Mbali na miili ya watu inayozidi 160 kutolewa kwenye vifusi lakini habari za majeruhi wangapi zikuwa baado hazijapatikana.

Oktoba mwaka wa 2005 tetemeko la ardhi lenye kipimo cha 7.6 lilitokea kaskazini magharibi mwa Pakistan pamoja na Kashmir na kusababisha vifo vya watu 74,000 na kuwaacha wengine 3.5 millioni bila makazi.

Mwaka wa 1935 tetemeko kubwa la ardhi liliwauwa takriban watu 30,000 katika eneo la Quetta.Wakati huo India ilikuwa chini ya utawala wa Uingereza.