1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Timu 16 zajikatia tikiti ya hatua ya mchujo

10 Desemba 2015

Michuano ya Klabu bingwa Ulaya – UEFA Champions League zimeingia sasa katika hatua ya mchujo baada ya timu 16 kujikatia tikiti katika mechi za mwisho za makundi

https://p.dw.com/p/1HLTJ
UEFA Champions League Bayer 04 Leverkusen vs. FC Barcelona
Picha: Getty Images/AFP/P. Stollarz

Katika mechi za kundi D, Bayer Leverkusen iligawana pointi na Barcelona kufuatia sare ya bao 1–1, Olympiakos wakiwa nyumbani dhidi ya Arsenal wakaambulia kichapo cha mabao 3-0 yaliyofungwa yote na Mfaransa Olivier Girioud.

Chelsea wakiwa katika ngome ya Stamford Bridge walijikatia tikiti kwa ushindi wa mabao 2 – 0 dhidi ya FC Porto, Valencia chini ya uongozi wa kocha mpya Garry Neville imechapwa bao 2 - 0 na Lyon,

FC Roma ilitoshana nguvu na BATE Borislov kwa kutoka sare ya kutofungana bao wakati miamba ya Ujerumani, Bayern Munich ikiichapa Dinamo Zagreb bao 2-0. Dynamo Kiev iliwafunga Macabbi Tel-Aviv bao 1–0 na KAA Gent ya Ubelgiji ikafunga kazi kwa kupata ushindi wa 2-1 dhidi ya Zenit ya Urusi.

Orodha kamili ya timu zilizofuzu katika hatua ya mchujo ya UEFA Champions League:

Timu zilizokuwa kileleni kwenye Makundi: Real Madrid, Wolfsburg, Atleico Madrid, Man City, Barcelona, Bayern Munich, Chelsea, Zenit

Timu zilizomaliza katika nafasi ya pili kwenye makundi: PSG, PSV, Benfica, Juventus, Roma, Arsenal, Dynamo Kiev, Gent.

Droo ya raundi ya muondowano ya timu 16 itafanyika Jumatatu Desemba 14.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman