1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Timu zaanza mazoezi kabla ya mkondo wa pili

Bruce Amani
2 Januari 2017

Ligi kuu ya kandanda hapa Ujerumani iko katika kipindi cha mapumziko ya msimu wa baridi na baada ya kuwa na likizo fupi ya sherehe za Krismasi timu zimeanza leo kuyaoa makali

https://p.dw.com/p/2V9oa
Fußball Bundesliga, FC Ingolstadt Training - Trainer Markus Kauczinski
Picha: picture-alliance/dpa/S. Puchner

Bayern watakuwa Doha kwa wiki moja ili kuwa tayari kwa awamu ya pili ya msimu itakayoanza Januari 20 ugenini dhidi ya Freiburg. Timu 15 kati ya 18 za Bundesliga zitakuwa na kambi za mazoezi nje ya Ujerumani, huku kumi zikipiga kambi Uhispania. Ni Cologne, Ingolstadt na Hoffenheim zitakazosalia hapa Ujerumani. Nambari mbili kwenye ligi RB Leipzig watakuwa katika kambi ya mazoezi mjini Lagos, Ureno.

Bayer Leverkusen wako Florida, Marekani kwa mwaka wao wa tatu mfululizo, wakati wachezaji wa Borussia Dortmund watakuwa na mapumziko marefu maana wataanza kufanya mazoezi yao Alhamisi mjini Marbella, Uhispania.

Borussia Moenchengladbach na washika mkia Darmstadt wataanza mwaka wa 2017 na makocha wapya. Aliyekuwa kocha wa Wolfsburg Dieter Hecking atachukua usukani kutoka kwa Andre Schubert katika klabu ya Gladbach wakati aliyekuwa kiungo wa Ujerumani Torsten Frings ataanza kazi yake ya kuifunza klabu ya ligi kuu kwa mara ya kwanza katika klabu ya Darmstadt.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri:Iddi Ssessanga