1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TOKYO: Waziri wa kilimo wa Japan ajiuzulu

3 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBT5

Waziri mpya wa kilimo wa Japan, Takehiko Endo, amejiuzulu kufuatia kashfa ya fedha inayomkabili.

Msemaji wa wizara ya kilimo mjini Tokyo amesema waziri mkuu wa Japan, Shinzo Abe, amekubali kujiuzulu kwa waziri huyo wa kilimo. Takehiko Endo amekiri alivunja sheria zinazohusiana na misaada ya serikali ya udhamini wa juhudi za kisiasa.

Endo alichukua wadhifa wake kama waziri wa kilimo Jumatatu wiki iliyopita kufuatia mabadiliko yaliyofanywa na waziri mkuu Shinzo Abe katika baraza lake la mawaziri.

Waziri huyo ni wa tano kujiuzulu katika baraza la mawaziri la Japan, mbali na wale walioondolewa kufuatia mabadiliko yaliyofanywa tangu Shinzo Abe alipochukua madaraka yapata mwaka mmoja uliopita.