1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TOKYO:Japan na Urussi kushirikiana katika nishati ya Nuklia

1 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCNi

Japan na Urussi zimekubaliana kuanza mazungumzo ya ushirikiano wa nishati ya Nuklia na kutia saini mikataba ya kukuza uhusiano wao wa kiuchumi.

Makubaliano hayo yamekuja katika mkutano baina ya waziri mkuu wa Urussi Mikhail Fradkov na mwenzake wa Japan Shinzo Abe mjini Tokyo Japan.

Mapatano hayo yanaweza kuihusisha Japan katika kutengeneza madini ya Uranium nchini Urussi kwa ajili ya viwanda vyake vya nishati ya Nuklia.

Viongozi hao wawili pia walijadili juu ya mzozo wa siku nyingi kuhusu maeneo ya visiwa kadhaa vya Pacific vinavyojulikana nchini Japan kama eneo la kaskazini na kusini Kuriles nchini Urussi. Lakini hakujakuwepo na dalili yoyote ya kufikiwa makubaliano juu ya suala hilo.

Mzozo wa maeneo hayo umesababisha Serikali hizo za Moscow na Tokyo kutoweza kusaini makubaliano ya amani kwa zaidi ya miaka 60 baada ya kumalizika vita vya pili vya dunia.