1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TRIPOLI: Steinmeier amesifu hatua za mabadiliko Libya

15 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCsk

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani,Frank-Walter Steinmeier,ziarani nchini Libya amesifu uelekeo wa mageuzi wa nchi hiyo.Steinmeier amesema,kipindi cha kutengwa miaka mingi kilimalizika,Libya ilipoamua kuacha kutengeneza silaha za maangamizi na kupinga ugaidi wa kila aina.Waziri Steinmeier alikuwa akizungumza mjini Benghazi katika sherehe ya kufungua mkutano wa uchumi wa Ujerumani na Libya.Akaongezea kuwa Libya sasa ni mfano kwa mataifa mengine. Steinmeier hii leo anaelekea Algeria.Vituo vingine vya ziara yake inayomalizika siku ya Jumamosi,ni Tunesia,Morokko na Mauritania.