1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump amekana mashtaka ya nyaraka za siri

Sudi Mnette
14 Juni 2023

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump amekana mashtaka yenye kuhusishwa makosa kadhaa ya ufujaji wa nyaraka za serikali. Hatua hiyo inamaanisha kwamba inaweza kuchukua mwaka mmoja au zaidi hadi kesi kuanza kusikilizwa.

https://p.dw.com/p/4SXdd
USA Prozess gegen Ex-Präsident Trump in Miami
Picha: Alon Skuy/Getty Images

Kesi hiyo ya kiserikali inasema Trump alihifadhi hati za usalama wa kitaifa kinyume cha sheria alipoondoka madarakani na kuwadanganya maafisa ambao walitaka kuzirejesha. Inadaiwa rais huyo wa zamani wa Marekani anatuhumiwa kuhodhi nyaraka za siri za serikali, kuwaonyesha wageni na kujaribu kuzificha dhidi ya timu ya wachunguzi.

Trump ambae anaonesha kuungwa mkono kwa kinyang'anyiro cha urais kwa mwaka ujao kwa chama chake cha Republican alijitokeza mwenyewe mahakamani kwa ajili ya kusikiliza kesi yake ambayo inatoa taswira ya namna yake katika jitihada ya kuwania tena urais.

Makosa 37 yahusishwa na Trump

Ikiwa ni takribani siku moja tu kabla kutimiza siku yake ya kuzaliwa, akiwa na umri wa miaka 77, Trump alifika mbele ya kizimba cha mahakama kuwasilishiwa rasmi makosa 37 chini ya mashtaka saba yaliyoletwa na wakili maalumu wa uchunguzi ambao ulifunguliwa baada ya Shirika la Ujasusi la Marekani FBI kufanya upekuzi katika makazi yake ya kifahariya  Florida miezi 10 iliyopita.

USA Prozess gegen Ex-Präsident Trump in Miami
Rais wa zamani wa Marekani Donald TrumpPicha: Brendan McDermid/REUTERS

Baada ya kutoka mahakamani Trump alikwenda kuzungumza na wafuwasi wake mjini New Jersey, ambapo pamoja na kumurushia maneno makali Rais Joe Biden alisema mashtaka yote yalioanishwa ni mambo ya kuundwa kama jitihada za kuingilia uchaguzi ujao wa taifa hilo wa mwaka 2024."Leo tunashuhudia utumiaji mbaya wa madaraka, mbaya katika historia ya nchi yetu. Jambo la kusikitisha sana kuona, rais fisadi anamkamata mpinzani wake mkuu wa kisiasa kwa tuhuma za uwongo ambazo yeye na marais wengine wangeweza kuwa pia na hatia,"alisema rais Trump.

Hoja ya rais kuwa na haki ya kuwa na nyaraka za siri

Amesema watu wanapaswa kutambua nyaraka zozote ambazo rais atahamua kuzichukua ana haki ya kufanya hivyo,na ni sawa kabisa, na hiyo ni sheria. Na hilo ndio linaloonekana sasa kwa wengi, na kuongeza kwa kusisitiza kuwa "wapaswa kuifuta kesi hiyo mara moja kwa sababu inavuruga nchi".

Trump anaungwa mkono sana na wapiga kura wa Republican, asilimia 81 ambao wanaamini kuwa mashtaka dhidi yake yanaendeshwa kisiasa.

Soma zaidi:Trump kufika tena mahakamani

Serikali ya Marekani  ambayo haijawahi kumshtaki rais yeyote wa zamani inamshutumu Trump kwa kukiuka Sheria ya Ujasusi na sheria zingine wakati aliondoa hati za siri alipoondoka madarakani mnamo 2021 na akashindwa kuzikabidhi kwa Hifadhi ya Kitaifa. Kesi hiyo inaweza kuwa na matokoa makubwa kisheria kwa kiwa na uwezekano wa hukumu ya miaka mingi gerezani.

Vyanzo: AFP/DW