1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump ashinda New Hampshire

Zainab Aziz
24 Januari 2024

Aliyekuwa rais wa Marekani, Donald Trump, ameshinda katika uchaguzi wa mchujo kwenye jimbo la New Hampshire.

https://p.dw.com/p/4bcHr
Trump / New Hampshire
Donald Trump amepata ushindi mwengine kwenye kura za mchujo kuwania uteuzi wa chama cha Republican kwenye uchaguzi wa rais wa Novemba 2024.Picha: TIMOTHY A. CLARY/AFP

Ushindi huo unamweka mbele bilionea huyo katika kinyanganyiro cha kumtafuta mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Republican.

Trump amemshinda mshindani wake aliyebakia katika kinyang'anyiro hicho, Nikki Haley, aliyekuwa balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa.

Kwa ushindi huo katika jimbo la New Hampshire,  Trump ameimarisha kwa kiwango kikubwa matumaini ya kuwa mgombea wa chama cha Republican katika uchaguzi wa rais wa Marekani mnamo mwezi Novemba.

Hata hivyo, mshindani wake Nikki Haley amesema amejizatiti kuendelea kushiriki katika uchaguzi wa mchujo wa chama cha Republican kwenye majimbo mengine.