1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump avurumuka na kuondoka mkutanoni kwa hasira

Sekione Kitojo
10 Januari 2019

Rais Trump wa Marekani anaelekea katika mpaka na Mexico ikiwa ni sehemu ya juhudi zake za kujenga ukuta,siku  moja baada ya kutoka katika mkutano wa majadiliano wakati wapinzani wa ujenzi huo kutoka chama cha Democratic 

https://p.dw.com/p/3BIL4
USA Washington Donald Trump
Picha: Getty Images/A. Wong

Donald  Trump  alivurumuka  na  kutoka  katika  mkutano  na viongozi wa  mabaraza  ya  bunge  la  Marekani " nilisema  kwaheri," aliandika  katika  ukurasa  wa  Twitter  muda  mfupi  baada  ya mkutano  huo, wakati  juhudi  za  kumaliza  kufungwa  kwa  sehemu shughuli  za  serikali, ziliingia  katika  mparaganyiko  mkubwa. Mamia kwa  maelfu  ya  wafanmyakazi  wa  serikali  wanakabiliwa   sasa  na kukosa  mishahara  hadi kesho  Ijumaa.

USA Washington Chuck Schumer und Nancy Pelosi nach Treffen mit Trump
Nancy Pelosi (katikati) akitoka katika mkutano na rais Trump katika Ikulu ya White house pamoja na Chuck Schumer (kushoto)Picha: picture-alliance/abaca/O. Douliery

Wakati  atakaposimama  kwa  muda  leo  mjini  McAllen , Texas , Trump atafanya  ziara  katika kituo  cha  mpakani  cha  doria  kwa ajili  ya mazungumzo kuhusiana  na  uhamiaji  na  usalama  wa mpakani, na  kupata  maelezo  kuhusu  usalama  wa  mpaka. Lakini Trump  ameelezea  shaka  shaka  yake  kwamba  kujitokeza  kwake pamoja  na  matamshi  hayatabadilisha  mawazo ya  mtu  yeyote, wakati  akitafuta  kupata  dola  bilioni 5.7 kwa  ajili  ya  ujenzi  wa ukuta ambao  umekuwa  ni  ahadi  yake  kuu  tangu  alipokuwa akifanya  kampeni  ya  urais.

Mazungumzo  hayo  yalizusha  uvumi  zaidi  juu  ya  iwapo  Trump atatangaza dharura  ya  kitaifa  na  kujaribu  kuidhinisha  ujenzi  wa ukuta  huo  binafsi  iwapo  baraza  la  Congress halitaidhinisha fedha  anazotaka.

USA Washington Donald Trump
Rais Donald Trump akielezea kuhusu mkutano wake mfupi na viongozi wa chama cha DemocraticPicha: Reuters/L. Millis

Mkutano  ulioparaganyika

Katika  siku  ya  19  ya  kufungwa  kwa  sehemu  ya  shughuli  za serikali  kulikosababishwa  na  kutokubaliana  kuhusiana  na  ujenzi wa  ukuta  huo, mkutano  mfupi kati  ya  Trump, kiongozi  wa maseneta  kutoka  chama  cha  Democratic Chuck Schumer  na spika  wa  baraza  la  wawakilishi  Nancy Pelosi  pamoja  na viongozi  wengine  ulimalizika  katika  mparaganyiko  na  hakuna ishara  ya  kupatikana  suluhisho.

"Alimuuliza spika Pelosi, "Unakubaliana  na  ukura  wangu?" Alisema hapana. na  alisimama  na  kusema  " kwahiyo  hakuna  cha  kujadili. "   na  aliondoka. "Na  tukliona  hasira  na  hamaki  kwasababu hakuweza  kupata  kile  anachotaka  na  aliondoka  tu kwenye mkutano.

USA Washington - 116th Vereidigungszeremonie des US Repräsentantenhaus
Jengo la bunge la Marekani Capital HillPicha: Getty Images/AFP/C. Somodevilla

Mkutano  huo  uliofanyika  katika  Ikulu  ya  White  House ulimalizika baada  tu  ya  dakika  14. Wademokrati  walisema walimuomba Trump  kufungua  serikali  lakini  aliwaambia  iwapo  atafanya  hivyo watampa  fedha  kwa  ajili  ya  ujenzi  wa  ukuta.

 Warepublikan  wamesema  Trump  aliuliza  swali  la  moja  kwa  moja kwa  spika  wa  baraza  la  wawakilishi  Nancy Pelosi , kwamba iwapo  atafungua  serikali , anaweza  kutoa  fedha  za  kugharamia ujenzi  wa  ukuta ?  Alisema  hapana. Trump  alikwenda  katika  jengo la  bunge mapema  jana  Jumatano, akitaka  kuwatuliza  wabunge wa  chama  chake  wasio  na  msimamo  thabiti. Na  aliondoka ajisifu  kuwa  chama  chake  kiko  pamoja  kabisa.

Mwandishi : Sekione  Kitojo  / ape

Mhariri: Caro Robi