1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump, Hilary wawinda katika majimbo muhimu

Bruce Amani
4 Novemba 2016

Wakati zikiwa zimesalia siku nne tu kabla ya Wamarekani kupiga kura, Hillary Clinton na Donald Trump walikabiliana jimboni North Carolina, kila mmoja akijaribu kunadi sera zake kwa Wamarekani

https://p.dw.com/p/2S8NW
Kombibild Trump Clinton
Picha: picture alliance/abaca/O. Douliery/newscom/N. Redmond

Huku wagombea wa urais wakitafuta umaarufu katika majimbo kadhaa muhimu ambayo yataamua matokeo uchaguzi wa Novemba nane, zawadi mbili kubwa kabisa kwenye ramani ya uchaguzi, Florida na North Carolina, sasa yanaonekana kuwa majimbo ambayo kura kwa wagombea hao zinakaribiana sana. Hayo ni kwa mujibu wa kampuni ya uchunguzi wa maoni ya RealClearPolitics.

Mgombea wa Democratic Hillary Clinton aliwatumia vigogo akiwemo Rais Barack Obama kuimarisha kampeni zake katika mkondo wa lala salama, wakati bilionea Donald Trump akimtupa mkewe Melania ulingoni ajaribu kuirekebisha hadhi ya Mrepublican huyo

Wagombea hao walizuru maeneo tofauti ya jimbo hilo la kusini mashariki ambako wote wana asilimia 46.4 kwa mujibu wa uchunguzi wa maoni.

"Nnajua kuna watu ambao wamekasirishwa kuhusu kilichofanyika katika kampeni hii. Watu huja na kuniambia, kuwa hawapati usingizi, kwamba matumbo yao yanawasumbua, wana maumivu ya kichwa. Na nadhani kuwa hiyo ni ishara muhimu, kwa sababu huu ni uamuzi muhimu": Amesema Hillary.

Picha za tume yxa uchaguzi Marekani kuwahimiza wananchi kupiga kura
Picha za tume yxa uchaguzi Marekani kuwahimiza wananchi kupiga kuraPicha: picture alliance/dpa/E. S. Lesser

Uchunguzi wa kitaifa wa CBS/New York Times uliongeza uongozi wa Bi Clinton unapungua kwa pointi tatu, na sasa ana asilimia 44 dhidi ya asilimia 42 ya Trump, ishara kuwa mfanyabiashara huyo tajiri anapata kura za wapiga kura warepublican ambao wakati mmoja walikuwa na mashaka kuhusu kampeni zake.

Trump leo anaelekea katika majimbo ya New Hampshire, Ohio na Pennsylvania, wakati Clinton akitua Ohio na Michigan. Kampeni ya mwisho ya Clinton itakuwa jimboni Philadelphia katika mkesha wa uchaguzi ambapo ataungana na mumewe Bill Clinton, Rais Barack Obama na mkewe Michelle Obama. Melania Trump, mwanamitindo mzaliwa wa Slovenia ambaye huenda akawa mama taifa wa kwanza mzaliwa wa kigeni katika karne mbili, pia alichagua Pennsylvania kufanya kampeni yake ya kwanza pekee yake

"Mimi ni mhamiaji, na acha niwaambie, hakuna anayethamini uhuru na fursa za Marekani zaidi yangu, kama mwanamke anayejisimamia na mtu ambaye alihamia Marekani. Mapenzi kwa taifa hili ni kitu kilichotuvutia wakati nilipokutana na Donald. Anapenda nchi hii, na anajua namna ya kuyatimiza mambo, sio tu kuzungumza" Amesema Melania.

Melania alisisitiza kuwa mumewe, anagombea kiti cha urais ili kuimarisha maisha ya wafanyakazi wanaoteseka na wazazi wanaoteseka kuwalea watoto wao

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Gakuba Daniel