1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump kutoongeza muda wa kujitenga

Sudi Mnette
30 Aprili 2020

Wakati Shirika la Fedha Duniani likiendelea kutangaza kuridhia fedha za dharura za kukabiliana na janga la corona, rais Donald Trump wa Marekani anasema hatoongeza muda wa miongozo ya watu kujitenga.

https://p.dw.com/p/3baQD
USA | Washington | Trump äußert sich über das Coronavirus
Picha: picture-alliance/Captital Pictures/MPI/RS

Pamoja na kukabiliana na upinzani kutoka pande tofati za taifa hilo, Rais Donald Trump wa Marekani amesema serikali haitozidisha muda wa mwisho wa miongozo ya kujitenga kwa raia wake baada muda wake uliopangwa Alhamisi hii kumalizika. Hata hivyo watu wake wa karibu akiwemo mshauri wake, Jared Kushner, wametabiri kwamba Marekani ambayo ipo katika hali mbaya ya kimaambukizi kwa wakati huu, hali hiyo inaweza kujirudia tena Julai. Wakati Marekani Trump anafikiria hatua hiyo huko Japan  Huko Japan kwa hivi sasa Waziri Mkuu Shinzo Abe anatarajiwa kuwasiliana na wataalamu kutathimini uwezekano wa kuongeza muda wa tangazo la hali ya hatari. Japan ina maambukizi 14,119 na vifo 435, lakini Marekani maambikizi  milioni 1.05 vifo 61.472.

IMF yaridhia fedha za dharura kwa mataifa 40 duniani.

Coronavirus Argentinien Essensausgabe für Arme
Watu wakipata msaa wa chakula nchini ArgentinaPicha: picture-alliance/AP/G. Garello

Katika hatua nyingine Shirika la Fedha Ulimwenguni limetangaza kuidhinisha fungu la kiasi cha dola milioni 650 kama fedha za dharura za uokozi kwa Jamhuri ya Dominik. Fedha hilo zitasaidia kufanya matumizi ya lazima ambayo yanahitajika kwa wakati huu pamoja na afya. Hilo ombi la 40 kuridhiwa na IMF katika kukabiliana na janga la virusi vya corona. Shirika hilo limesema zaidi wa mataifa wanachama 100, miongoni mwa mataifa 189 ya shirika hilo yameomba fedha.

Maambukizi ya virusi yaongezeka Ujerumani.

Deutschland Coronavirus Maskenpflicht
Raia wa Ujerumani akijipatia huduma ya barakoaPicha: Reuters/A. Schmidt

Ujerumani maambukizi 1,478 yameongezeka na kufanya jumla ya 159,119. Na vifo vilivyotoka na virusi hivyo vimengezeka 173 ikilinganishwa na jana na hivyo kufikia vifo 6,288. Na Kwa mara ya kwanza Korea ya Kusini imesema hakuna ripoti mpya ya kisa cha maambukizi ya ndani tangu kuripuko kwa ugonjwa huo Februari. Jana kuliripitwa visa vipya vinne na vyote kutoka nje ya taifa hilo na hivyo kufanya juma la maambukizi 10,765 na vifo 247.

Nchini China kumeripotiwa visa vipya vinne vya maambukizi ya virusi vya corona kwa Aprili 29, ikiwa ni pungufu ya vingine 22 vilivyobanika siku moja kabla. Kwa mujibu wa mamlaka ya afya ya nchi hiyo visa vyote hivyo ni kutokoka mataifa ya nje. Idadi jumla ya maambukizi hadi wakati huu imefikia watu 82,862, pasipo na kisa kipya cha kifo. Huku jumla ya vifo ikisalia 4,633.  Na kwa mara ya kwanza Yemen kumeripotiwa vifo viwili vilivyotokea katika mji wa bandari wa Aden. Jumanne Iliyopita Umoja wa Mataifa ulisema upo uwezekano wa virusi vya corona kusambaa katika mji ya taifa hilo lililovurugwa kwa vita.