1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump na Seneti kujadili msaada wa kupambana na COVID-19

Admin.WagnerD20 Julai 2020

Viongozi wakuu wa chama cha Republican katika Bunge la Marekani wanatarajiwa kukutana na rais Donald Trump kujadili mpango mwingine wa msaada wa kifedha unaonuwia kupunguza mtikisiko uliosababishwa na janga la COVID-19.

https://p.dw.com/p/3faX4
Washington: Das Kapitol - Sitz des US-Kongresses
Picha: picture-alliance/J. Schwenkenbecher

Mkutano huo utakaofanyika katika Ikulu mjini Washington umeitishwa wakati matumaini ya wamarekani kuwa janga la virusi vya corona linaelekea ukingoni yameporomoka baada ya kuzuka wimbi jipya la maambukizi nchini humo.

Migawanyiko baina ya viongozi wakuu wa chama cha Republican katika Baraza la Seneti na Ikulu ya Marekani inatishia kuleta changamoto mpya katika kushughulikia kadhia ya corona.

USA Washinton | Mehrheitsführer im Senat Mitch McConnell
Kiongozi wa Republican katika Baraza la Seneti, Mitch McConnellPicha: Reuters/U.S. Senate TV

Kiongozi wa Republican katika Baraza la Seneti Mitch McConnell anataka kuweko mpango mwingine wa uokozi wa dola Trilioni moja katika siku chache zinazokuja lakini utawala wa rais Trump wenyewe unatoa kipaumbele katika kuongeza fedha za kuimarisha upimaji wa virusi vya corona.

Hapo jana rais Trump alilisitiza kuwa virusi vya corona vitatokomezwa hivi karibuni lakini maoni yake yanatofautiana na makadirio ya wataalamu wa afya wanaotiwa wasiwasi na ongezeko la visa vipya na vifo vya COVID-19 nchini Marekani.  

Wakati visa jumla vya maambukzii ya virusi vy corona imefikia milioni 14 kote duniani, Marekani yenyewe tayari imerikodi visa 3,762,081 nchini nzima na jana Jumapili ilitangaza maambukizi mapya 60,000 katika kipindi cha saa 24 zilizotangulia.

Hali hiyo inaamanisha ni muhimu kuwa na mpango mwingine wa uokozi kwa sababu biashara zilizoanza kufunguliwa zinalazimika kufungwa tena kwa sababu ya wimbi jipya la maambukizi.

Mataifa mengine hali ni bado ni tete

Nchini India moja ya taifa lililoathiriwa sana na janga la COVID-19 serikali imetangaza leo visa vipya 40,000 vya virusi vya corona vilivorikodiwa katika muda wa saa 24 zilizopita.

Idadi hiyo ambayo ni kubwa zaidi kuwahi kuripotiwa inafanya India kufikia visa 1,118,043 na vifo 27,497 vya COVID-19.

Wakati hayo yanajiri barani Asia, nchini Brazil, taifa la Amerika ya Kusini idadi ya vifo vya COVID-19 inaelekea kufikia 80,000 baada ya watu 716 kupoteza maisha siku ya Jumamosi pekee.

Indien | Coronavirus
Picha: Getty Images/AFP/N. Seelam

Idadi ya maambukizi ilifikia visa 2,098,389 jana Jumapili na kuifanya nchi hiyo kuwa ya pili duniani kwa mamabukzii makubwa baada ya Marekani.

Huko China, mripuko mpya wa virusi vya corona umesambaa katika mji wa pili wa mkoa wa Kaskazini Magharibi wa Xinjiang.

Mamlaka za eneo hilo ambalo lilishuhudia athari kidogo wakati janga la COVID-19 lilipotandaa mwanzoni mwa mwaka 2020 zinajaribu kuzuia kusambaa virusi kwa kutangaza marufuku kali zinazozuia watu kutoka nje.

Hata hivyo Shirika la Afya duniani WHO limetoa taarifa za matumaini kuwa chanjo ya virusi vya corana itaanza kutolewa kwa watu wengi ifikapo katikati ya mwaka ujao.

Mwanasayansi kiongozi wa WHO Soumya Swaminathan  amesema hivi sasa kuna matumaini kutoka utafiti wa chanjo 20 zinazoendelea na majaribioo lakini amesema matumaini yote hayo yanategemea hatua za kitafiti na utengenzaji wa chanjo hizo utakavyokuwa.

Mwandishi: Rashid Chilumba

Mhariri: Charo Josephat