1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tshisekedi ateua kamanda mpya operesheni za kijeshi

6 Septemba 2023

Rais Felix Tshisekedi amemtea Chaligonza Nduru kuwa kaimu gavana na kamanda wa operesheni za kijeshi katika mkoa wa Kivu Kaskazini akichukua nafasi ya Luteni Jenerali Constant Ndima.

https://p.dw.com/p/4W0Mu
FARDC
Askari wa jeshi la Kongo-FARDCPicha: Alain Wandimoyi/AFP

Hayo yanajiri  wakati huu ambapo kesi ya wanajeshi 6 waliohusika katika ukandamizaji  mbaya dhidi  ya maandamano  ya raia, ikianza kusikilizwa tangu Jumanne na mahakama kuu ya kijeshi mjini Goma. Washtakiwa hao ni maafisa wawili wa jeshi la FARDC, kanali Mike Mikombe na Luteni kanali Donatien Bawili ambao serikali ilitangaza  kuwakamata pamoja na askari wa nne wa vyeo vya chini.

Hata hivyo, mashirika ya kiraia katika mji huu wa Goma yanayopoteza matumaini kwa vyombo vya usalama, yameomba kuondolewa mara moja kwa  uongozi huo wakijeshi wanaoutuhumu kuhusika na visa vya uhalifudhidi ya raia hasa wakati huu ambako zaidi ya watu 150 ambao ni waumini wa dhehebu la kizalendo wanaendelea kuzuiliwa korokoroni, Mario Ngavo ni afisa mkuu wa asasi za kiraia mjini Goma .

Asakri wa Kongo Beni
Wanajeshi wa Kongo katika operesheni za MasharikiPicha: Alain Uaykani/Xinhua News Agency/picture alliance

Wakati huo huo, serikali imemtangaza Jenerali Chaligonza Nduru kuwa kaimu gavana wa kijeshi na kamanda wa operesheni za kijeshi zinazoendelea kurejesha usalama mkoani humo, akichukuwa nafasi ya Lt.Constant NDIMA ambaye amerejesha mjini Kinshasa kwa mahojiano. Aidha, raia hao wanaoendelea kuwakumbuka wapendwa wao waliofariki katika maandamano hayo kwakupigwa risasi, waelezea hisia zao.

Hatua hiyo ya serikali,imejiri baada ya ujumbe wa mawaziri kutoka kinshasa kumaliza ziara yao hapa mjini  Goma ambako waliahidi kutoa mwanga juu ya tukio hilo la Agosti 30.