1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tumeukaribisha mwaka mpya 2013

1 Januari 2013

Mwaka mpya wa 2013 umekaribishwa kwa aina yake duniani kote,wakati mamilioni ya watu wakimiminika katika bandari ya mjini Sydney nchini Australia,eneo la sherehe mjini Berlin na mjini London kuangalia fashifashi.

https://p.dw.com/p/17Bmv
Spectator boats in Sydney Harbour look on as New Year's Eve fireworks erupt over the Sydney Harbour Bridge on January 1, 2013. Sydney kicked off a wave of dazzling firework displays welcoming in 2013, from Dubai to Moscow and London, with long-isolated Yangon joining the global pyrotechnics for the first time. AFP PHOTO/MANAN VATSYAYANA (Photo credit should read MANAN VATSYAYANA/AFP/Getty Images)
Fashifashi zikirushwa angani mjini Sydney australiaPicha: Getty Images

Baadhi ya watu waliokusanyika kusherehekea walijikusanya katika maeneo tulivu , wakivalia mavazi nadhifu ya kimono ama kula vyakula wavipendavyo.

Pia kulikuwa na tukio lililozoeleka la kuweka tufe la dunia katika uwanja wa Times mjini New York , sherehe ambazo zilichafuliwa na kifo mwaka jana cha Dirk Clark , mshauri maalum wa muziki wa rock ambaye kwa miaka kadha amekuwa akisimamia sherehe hizo katika televisheni moja ya Marekani licha ya kuathirika na ulemavu uliosababishwa na ugonjwa wa kiharusi.

Fireworks explode over Dresden's Church of Our Lady (Frauenkirche) on New Year's Eve on December 31, 2012 in Dresden, eastern Germany. AFP PHOTO / ROBERT MICHAEL (Photo credit should r... Erfahren Sie mehr
Fashifashi zikirushwa angani kuukaribisha mwaka mpya mjini BerlinPicha: Getty Images

Mjini Berlin

Mjini Berlin , mamia kwa maelfu ya watu waliokuwa wakifurahia waliunganisha mikono yao katika mitaa iliyojaa watu katika juhudi zao za kutaka kuvunja rekodi ya dunia kwa kucheza midundo ya muziki maarufu wa Gangnam style, uliopigwa na mwanamuziki kutoka Korea ya kusini kwa muziki wa kufoka foka Psy. Gangnam , na wachezaji hao walicheza kwa kufuatia mirindimo ya kuhesabu dakika kuelekea mwaka mpya.

Watu wanaokadiriwa kufikia milioni moja walifurika katika eneo maarufu mjini Berlin la sherehe, ambako wanamuziki wa kundi la Pet Shop Boys walitumbuiza na dakika 11 za kurusha fashifashi angani zilikuwa kivutio kikubwa.

Mitaa kuelekea lango kuu la Brandenburg ilikuwa imefurika watu na ilikuwa ni vigumu mtu kuweza kupita kirahisi hata katika saa kabla ya sherehe hizo. Majira ya usiku wa manane , fashifashi 6,000 zilirushwa angani zikisikika kwa sauti kishindo kikubwa na rangi mbali mbali za kupendeza. Jiji hilo la Berlin lilisikika sauti za kuripuriwa kwa fashifasi mchana kutwa.

Mwaka waanza Australia

Mwaka ulianzia mjini Sydney , ambako zaidi ya watu milioni moja waliokuwa wakijiburudisha walijazana katika bandari ya mji huo kwa ajili ya kuona tukio maarufu la onyesho la kurushwa kwa fashifashi ambalo linakamilisha sherehe za kuukaribisha mwaka mpya na kisha kusogea upande wa magharibi kuifunika dunia yote.

SYDNEY, AUSTRALIA - DECEMBER 31: Fireworks light up the sky during the nine o'clock show during New Years Eve celebrations on Sydney Harbour on December 31, 2012 in Sydney, Australia. (Photo by Cameron Spencer/Getty Images)
Fashifashi katika bandari ya mji wa SydneyPicha: Getty Images

Watu waliotembelea mji huo mkubwa nchini Australia waliburudishwa na miripuko 100,000 ya fashifashi kutokana na tani saba za fashifashi zilizowekwa katika daraja na matishari bandarini hapo.

Mwanamuziki nyota wa muziki wa pop, Kylie Minogue aliongoza hesabu ya dakika za mwisho kuelekea mwaka mpya akiliongoza kundi la watu waliokuwapo katika eneo hilo ambapo watayarishaji wa sherehe hizo wanasema zinaweza kuzidi zile zinazofanyika kila mwaka mjini New York , mjini London na Berlin.

BBC handout photo issued Saturday Dec. 1 2001 of Australian singer Kylie Minogue reacting after winning the Best Single Award at the Manchester Evening News Arena, during the first ever Top Of The Pops Awards Friday November 30 2001. (AP Photo/Mark Allan/BBC)
Mwanamuziki Kylie Minogue akitumbuiza

Nchini Ufilipino , mahospitali yaliwekwa katika hali ya tahadhari wakati maafisa wakitoa miito ya dakika za mwisho ya kuachana na taratibu za kawaida za kufyatua fashifashi na kufyatua risasi hewani.

Wafilipino wafukuza bahati mbaya ya mwaka jana

Wafilipino kwa kawaida hufanya kelele nyingi, ikiwa ni pamoja na ufyatuaji wa fashifashi, katika sherehe za kuukaribisha mwaka mpya kwa imani kuwa wanaifukuza bahati mbaya ya mwaka uliopita na kuvutia bahati nzuri katika mwaka mpya. Baadhi ya watu wanaosherehekea hufyatua risasi hewani.

Empty champagne bottles and glasses are pictured during a New Year's Eve celebrations in Vienna December 31, 2012. REUTERS/Lisi Niesner (AUSTRIA - Tags: SOCIETY ANNIVERSARY)
Vinywaji wakati wa kuukaribisha mwaka mpya 2013Picha: Reuters

Nchini Japan , ambako watu wengi wamegeukia dini kutokana na nchi hiyo kutumbukia katika mdororo wa uchumi mwaka jana wa 2012, watu wameanza kufurika katika maeneo ya ibada kusali wakiomba ufanisi na afya njema.

kiasi ya watu milioni 100 wanatarajiwa kutembelea maeneo ya ibada katika muda wa siku tatu zijazo.

Mwandishi : Sekione Kitojo / dpae

Mhariri: Stumai George