1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TUNIS: Mamia ya watu waandamana kulaani kunyongwa kwa Saddam

3 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCdm

Mamia ya watu walifanya maandamano mjini Tunis nchini Tunisia kulaani kunyongwa kwa rais wa zamani wa Irak, Saddam Hussein.

Viongozi wa chama cha wafanyakazi nchini humo wameilaumu Marekani na Uingereza wakisema zinabeba dhamana kwa kitendo hicho ambacho huenda kikaifanya hali nchini Irak kuwa mbaya.

Waandamanaji hao walikusanyika nje ya makao makuu ya chama cha wafanyakazi wakiwa wamebeba picha za Saddam Hussen na kupiga kelele za kumtaja Saddam kuwa shahidi na kuilaani Marekani.

Wakili aliyemtetea Saddam mahakamani, raia wa Tunisia, Ahmed Saddiq, alihutubia mkutano wa hadhara mjini Tunis na kuwahimiza waandamanaji wamkumbuke Saddam kama shujaa badala ya kumlilia.