1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Twitter yairejesha akaunti ya Trump

20 Novemba 2022

Mmiliki mpya wa mtandao huo wa kijamii Elon Musk ameirejesha akaunti ya Rais huyo wa zamani wa Marekani

https://p.dw.com/p/4Jn8Y
USA | Trump will bei Wahl 2024 erneut antreten
Picha: Octavio Jones/REUTERS

Mtandao wa kijamii wa Twitter umeirejesha akaunti ya rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump. Hayo yameelezwa usiku wa kuamkia leo na mmiliki mpya wa Twitter, Elon Musk.

Akaunti ya Trump iliyokuwa imefungwa kwa muda wa miezi 22, ilionekana tena kwenye mtandao huo jana Jumamosi.

Elon Musk schließt Twitter-Pleite nicht aus
Elon Musk, Mmiliki mpya wa mtandao wa kijamii wa TwitterPicha: Mike Blake/REUTERS

Musk aliendesha kura ya maoni, ambapo watumiaji milioni 15 wa Twitter walipiga kura, huku asilimia 51.8 wakipiga kura ya ndiyo.

Akaunti ya Trump ilisimamishwa mwezi Januari, 2021, siku mbili baada ya wafuasi wake kuyavamia majengo ya bunge la Marekani na kusababisha kikao cha bunge la pamoja kusitishwa pamoja na vifo vya watu watano.

Wafuasi hao walikuwa na nia ya kuzuia kupitishwa matokeo ya uchaguzi wa urais wa mwaka 2020 yaliyompa ushindi Rais wa sasa wa Marekani Joe Biden. Hivi majuzi, Trump alitangaza nia yake ya kugombea tena urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2024.

USA Trumps neue Social Media Plattform "Truth social"
Mtandao mpya wa kijamii wa Trump unaoitwa "Truth"Picha: Muhammad Ata/ZUMAPRESS.com/picture alliance

Mapema leo, Trump amesema hana haja ya kurejea kwenye Twitter na badala yake atasalia katika mtandao wake wa kijamii  aliyouanzisha wa "Truth".