1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi nchini Sierra Leone

13 Agosti 2007

Shughuli za kuhesabu kura inaendelea nchini Sierra Leone baada ya uchaguzi kufanyika mwishoni mwa juma lililopita.

https://p.dw.com/p/CH9i
Raia wa Sierra Leone wakisubiri kupiga kura.
Raia wa Sierra Leone wakisubiri kupiga kura.Picha: AP
Huu ni uchaguzi wa kwanza kufanyika tangu wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa kuondoka miaka miwili iliyopita. Wapiga kura wengi walijitokeza kumchagua kiongozi wa taifa na wabunge. Rais Tejjan Kabah anamaliza kipindi chake cha uongozi baada ya kuwa madarakani tangu mwaka 2002 wakati vita vya wenyewe kwa wenyewe vilipokwisha. Vita hivyo vilidumu kwa miaka 11 na kuendelezwa na almasi. Ili kupata picha kamili Thelma Mwadzaya amezungumza na Said Msonga mkaazi wa Freetown, Sierra Leone.