1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi Ulaya: Vyama vikuu vyapata pigo, Kijani wapeta

Iddi Ssessanga
26 Mei 2019

Matokeo ya uchaguzi wa bunge la Ulaya yanaonyesha vyama vikongwe vya mrengo wa kati vimepoteza kura nyingi huku vyama vya kijani vikiongeza uwakilishi wake.

https://p.dw.com/p/3J8dw
Eurpawahl Die Grünen Jubel
Picha: Getty Images/AFP/T. Schwarz

- Jumapili ndiyo ilikuwa siku ya mwisho ya uchaguzi wa Umoja wa Ulaya. Mataifa 21 yalishiriki zoezi hilo.

- Nchini Ujerumani muungano tawala wa vyama vya siasa za wastani za mirengo ya kulia na kushoto vimeshuhudia  uungwaji wake mkono ukiporomoka vibaya huku chama cha Kijani kinachotetea mazingira kikiibuka katika nafasi ya pili.

- Kashfa ya karibuni nchini Austria ambayo ilisababisha kuvunjika kwa serikali haijawazuwia wapigakura kuviunga mkono vyama vilivyoshirikiana katika serikali ya muungano vya People's Party (OeVP) na kile cha Freedom Party (FPOe).

Matokeo kama yanavyoingia

20:50 Makadirio ya kwanza ya Bunge la Ulaya yanaonyesha kuwa vyama vikuu vimepoteza pakubwa katika uchaguzi wa bunge la Ulaya, huku vyama vya watetezi wa Mazingira vya Kijani na vile vya siasa kali za mrengo wa kulia vikitazamiwa kuongeza idadi yake ya viti vya uwakilishi.

Infografik HOCHRECHNUNG 19.59 EU Wahl 2019 - Deutschland KIS

Makadirio kutoka katika mataifa 11 ya Umoja wa Ulaya na nia za upigaji kura katika mengine 17, yanaonyesha kuwa kambi ya mrengo wa wastani wa kulia ya European People's Party EEP, itandelea kuwa kambi kubwa zaidi ikiwa na viti 173, kutoka viti 217 ilivyopata mwaka 2014.

Kambi ya mrengo wa wastani wa kushoto itapoteza viti 40, na kushuka hadi viti 147. Kambi ya mrengo wa kushoto ya vyama vya Kijani inatazamiwa kushinda viti 71, idiadi hii ikiwa imeongezeka kutoka viti 52 mwaka 2014.

Kundi la European of Nations and Freedom, linalounganisha vyama vya siasa kali za mrego wa kulia katika mataifa kama Ufaransa na Italia, linaonekana kujipatia viti 57, kutoka 20 miaka mitano iliyopita.

Licha ya hasara hiyo, vyama vikuu na vile vinanyounga mkono kwa nguvu Umoja wa Ulaya vinatizamiwa kushindi jumla ya viti 493 kati ya viti 751 bungeni.

20:40 Makadirio ya kwanza ya mgawanyo wa viti yanathibitisha kuvunjika kwa muungano mkuu kati ya kambi ya mrengo wa wastani wa kulia ya European People's Party (EEP) na ile ya mrengo wa wasatani wa kushoto ya S&D.

18:14 Manfred Weber, mwanasiasa wa chama wa CDU ambaye aliteuliwa kuwa mgombea wa nafasi ya rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya kupitia kambi ya EEP, alisema uitikiaji mkubwa wa wapigakura katika kanda hiyo ndiyo habari muhimu zaidi kutoka katika uchaguzi huo.

"Ni uimarishaji wa wazi wa bunge la Ulaya katika majadiliano yanayokuja," Weber alisema. "Bunge la Ulaya ndiyo mahala ambako raia wa Ulaya wanawakilishwa, na sasa linapaswa kuwa na ushawishi unaolingana kwenye maamuzi yanayohusu masuala na watumishi kwenye ngazi ya Ulaya."

Chanzo: mashirika