1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi wa bunge nchini Lebanon mwezi Juni

1 Mei 2009

Ushawishi wa Koo za wanasiasa waliouawa bado ungalipo

https://p.dw.com/p/Hi79
Beshir Gemayel aliyewahi kuwa rais wa Lebanon.Picha: picture-alliance/ dpa

Wagombea wanaotokana na koo za viongozi waliouawa nchi ni Lebanon, wanatarajiwa kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa bunge nchini humo mwezi Juni mwaka huu, wakitoa sura sawa na ule utamaduni wa ukoo wa Kennedy katika jukwaa la kisiasa nchini Marekani . zaidi anayo Mohamed Abdul-Rahman◄

Koo za viongozi wa zamani waliouawa nchini Lebanon bado zina ushawishi mkubwa katika jamii zao. Nadim Gemayel mwenye umri wa miaka 27 ni mtoto wa rais aliyeuwawa Beshir Gemayel. Ni kutoka familia ya kikristo ya madhebu ya Maronite ilioanzisha chama cha Phalange cha siasa za mrengo wa kulia 1936 na kubakia tangu wakati huo katika safu ya usoni ya siasa za Lebanon hata kupachikawa jina la utani " Kennedy wa Lebanon."

Beshir na nduguye Amin Gemayel walikua viongozi wakuu wa taifa hilo. Mjane wa Beshir ni mbunge hivi sasa lakini hatogombea uchaguzi mwezi jJuni akitumai kwamba mwanawe wa kiume Nadim atachukua nafasi hiyo.

Mtoto wa kiume wa Amin Gemayel, Pierre alikua waziri wa viwanda 2005, kabla ya kuuawa mwaka mmoja baadae.

Kukamilisha sura hiyo, mtoto pekee wa kiume wa Amin, Sami pia atagombea kiti cha ubunge katika uchaguzi wa Juni 7 .

Kurithishiana nafasi za kisiasa kwa miongo kadhaa limegeuka kuwa jambo la kawaida nchini Lebanon.

Michel Moawad mtoto wa rais wa zamani Rene Moawad aliyeuwawa 1989 pia ameingia katika ulingo wa kisiasa akishawishiwa na mama yake Nayla ambaye amewahi kuwa waziri na sasa ni mbunge.

Wakati baba yake alipouwawa Michel alikua na umri wa miaka 17 akisoma nchini Ufaransa.

Sleiman Frangieh ni mtoto awa kiume wa rais mwengine awa zamani. Babu yake Tony Frangieh alikua waziri na aliuawa 1978 wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Lebanon vilivyodumu miaka 15.

Mbunge Walid Jumblat atapigania tena kiti chake cha ubunge kutokana na kurithi uongozi wa chama cha na jamii ya Wadruze kutoka kwa baba yake Kamal -mwanasiasa wa kihistoria ambaye pia aliuawa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe 1975-1990.

Saad Hariri Sohn des ehemaligen Ministerpräsidenten des Libanons
Saad Hariri,mtoto wa Waziri mkuu wa zamani Rafiq HaririPicha: AP

Miongoni mwa Wasunni Saad Hariri amechukua uongozi wa kundi lenye wajumbe wengi bungeni tangu 2005 alipouawa baba yake tajiri mkubwa na waziri mkuu wa zamani Rafiq hariri aliyeshika wadhifa huo mara tano.

Ni chama cha Washia Hezbollah kinachoongozwa na Hassan Nasrallah kikiwa pia na tawi la kijeshi, ambacho kinajisifu kwa kutochanganya siasa na mafungamano au ushawishi wa kifamilia.

Lakini mshirika wake Mkristo Jenerali mstaafu Michel Aoun na mkwe wake wa kiume ambaye yuko serikalini akiwa waziri wa mawasiliano, wakati mke wa mpinzani wake Samir Geagea,Sethrida ni mbunge.

Kwa wapiga kura wengi nchini Lebanon mfumo wa kisiasa umewachosha na kuna hali ya kutoridhika na kinachotokea hivi sasa. Wengi wanasema kila mtu anapaswa kuwa na haki ya kugombea ubunge na mtindo wa kuwapa kipa umbele au kuwaachia nafasi watoto wa viongozi na wajukuu wao hauna budi kukomeshwa.

Fadia Kiwan kutoka idara ya sayansi ya siasa katika chuo kikuu cha Saint Joseph mjini Beirut anasema wagombea wapya kutoka koo maarufu kisiasa hawana budi kuyashawishi majimbo yao kuwa wanaweza kusimama wao wenyewe bila kutumia ushawishi wa koo zao. na zaidi ya yote wawe na fikra mpya, kwa sababu kinachowazunguka ni kivuli cha baba au babu zao waliouawa.

Mwandishi: Abdulrahman Mohamed/AFPE

Mhariri. Josephat Charo