1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi wa bunge Timor ya Mashariki wapita salama

30 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBn0

Dili:

Wapiga kura wa Timor ya mashariki wameteremka vituoni kulichagua bunge lao la pili tangu uhuru mwaka 2002,kufuatia machafuko ya mwaka jana yaliyogharimu maisha ya watu 37.Uchaguzi umepita salama-maafisa wa umoja wa mataifa wamethibitisha.

Matokeo ya awali yanatarajiwa kutangazwa wiki ijayo.Vyama 14 vinapigania viti bungeni huku chama tawala cha FRITILIN kikikabiliwa na upinzani mkubwa kutoka chama kipya kilichoundwa na rais wa zamani Xanana Gusmao.Hakuna hata kimoja kinachotazamiwa kujikingia wingi wa viti katika bunge lenye viti 65 kuweza kuunda serikali bila ya ushirikiano.Rais Jose Ramos Horta amewatolea mwito wakaazi wa kisiwa hicho kidogo chenye wananchi milioni moja waungane na kuupiga vita umaskini-