1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi wa rais nchini Iran

20 Mei 2009

Baraza la uchaguzi nchini Iran lawaidhinisha watetezi 4 kugombea urais Juni 12.

https://p.dw.com/p/HuDn
Mahmoud Ahmadinejad.Picha: AP

Kiongozi wa Iran mwenye msimamo mkali Mahmoud Ahmadinejad anakabiliwa na upinzani mkali wa mhafidhina mwenzake, mgombea wa siasa za wastani na mawana mageuzi katika mchuano wa wagombea wanne wa uchaguzi ujao wa rais nchini humo, utakaofanyika tarehe 12 mwezi ujao wa Juni- hayo ni kwa mujibu wa orodha ya mwisho ya wagombea waliodhinishwa jana. Ramadhan Ali anaripoti kamili .

Mbali na Ahmadinejad, wale walioidhinishwa kugombea wadhifa wa urais hapo juni 12 na baraza la uchaguzi ni mkuu wa zamani wa kikosi cha walinzi wa mapinduzi,mohsen Rezai,waziri mkuu wa zamani Mir Hossein Mousavi na spika wa zamani wa Bunge Mehdi Karroubi-hii ni kwa muujibu alivyotangaza waziri wa ndani Sadeq M ahsouli.

"kuanzia sasa wote hao wanaweza kuanza kampeni ya uchaguzi hadi masaa 24 kabla ya siku ya kupigwa kura."

Jumla ya wairani 475 walijiandikisha kuwa watetezi katika uchaguzi huo wa rais kati yao wanaume 433 na wanawake 42.Na wote walichunguzwa na Baraza la uongozi lenye nguvu la wajumbe 12 , likijumuisha viongozi 6 wa kidini walioteuliwa na Kiongozi mkuu na wanasheria 6 waliopendekezwa na mkuu wa Idara ya sheria.

Baraza la uongozi mwishoe likawaidhinisha watetezi 4.

Katika uchaguzi wa 2005 ambao mshindi alikuwa rais wa sasa Ahmadinejad ,watetezi 8 kati ya wote 1,014 waliojiandikisha waliidhinishwa na baraza hilo na mwishoe ni watetezi 7 tu waliopita kugombea.

Katika kipindi chake cha miaka 4,rais Ahmadinejad amepata umaarufu ulimwenguni kwa matamshi yake makali dhidi ya Israel na kuwa m kakamavu wa kuregeza ka mba katika mradi wa nuklia wa Iran.Sera zake za uchumi lakini zimemfanya abishwe nyumbani Iran.

Rezai,mhafidhina na mkosoaji wake anaedai anagombea uchaguzi huu kama mtetezi huru, aliviongoza vikosi vya wanamapinduzi wa Iran miaka 16 iliopita na anajulikana kwa rekodi yake ya msimamo mkali.Amekuwa akimkosoa mno rais wa sasa Ahamdinejad.Mousavi anaedai kuwa ni mfanya-mageuzi anaeegemea kanuni za mapinduzi ya kiislamu ya 1979,ameahidi kuwa, endapo akichaguliwa atajitahidfi kubadili sura ya Iran kuwa si dola lenye siasa kali kinyume na wakati wa utawala wa rais wa sasa Ahmadinejad.

Karroubi,spika wa zamani wa Bunge la Iran,ndie mpenda mno maguezi kati ya watetezi wote 4,lakini anasisitiza kuwa atakuwsa muangalifu katika kufanya m,abadiliko ili asiwakere wakakamavu ndani ya utawala wa Iran.

Kiongozi mkuu wa kidini wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, alijitokeza wazi wiki hii kumuungamkono Ahamdinejad na kuwashawishi wapigakura kutomchagua mtetezi atakaeelemea kambi ya magharibi.

Wairani milioni 46.2 wana haki ya kupigakura.

Muandishi:Ramadhan Ali /AFPE

Mhariri: M.Abdulrahaman