1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi wa Ulaya na Lebanon na kuyumbishwa waziri mkuu Brown:

9 Juni 2009

Brown amevuka salama alao kwa sasa:

https://p.dw.com/p/I6Br
Waziri mkuu Brown

Maoni ya wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo yamechambua tangu mada za ndani hata za nje ya nchi: Ndani, yamezungumzia pigo la chama cha SPD katika uchaguzi wa Bunge la ulaya na pia juu ya juhudi za kuliokoa kampuni la Karstadt kutofilisika na kupoteza nafasi za kazi kwa watumishi wake. Nje, kunusurika kuanguka jana kwa waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown na juu ya matoeko ya uchaguzi wa Lebanon.

Gazeti la FINANCIAL TIMES DEUTSCHLAND juu ya matokeo ya uchaguzi wa Lebanon :

"Habari za kusangaza zikija kutoka Mashariki ya Kati, mara nyingi huwa habari mbaya.Matokeo ya uchaguzi wa Lebanon lakini, ni kinyume na desturi hiyo.Ushindi wa kambi inayoelemea nchi za magharibi katika uchaguzi wa Lebanon, ni tukeo la kusangaza kweli na wakati huo huo habari nzuri kwa eneo zima la mashariki ya Kati.

Hii haina maana matatizo yote ya Lebanon sasa yamepatiwsa ufumbuzi la hasha.

Muda uliopita sura ilioibuka Mashariki ya kati ni ya siasa kali kila upande-kuanzia kunyakua madaraka kwa chama cha Hamas katika Gaza hadi kuchaguliwa kwa serikali yenye iasa kali za mrengo wa kulia nchini Israel ambayo haikubakliani na ufumbuzi wa kuwa na dola mbili-yao na ile ya wapalestina.

Laiti Lebanon nao ingetumbukia katika shimo hilo hilo,basi hilo lingekuwa pigo jen gine kali kwa matumaini ya amani."

Gazeti la SAARBRUCKER ZEITUNG linachambua hatima ya waziri mkuu wa Uingereza, Gordon Brown na jinsi alivyovuka chupu-chupu jana kuanguka:

"Gordon Brown, hana nafasi,lakini anaitumia nafasi asionayo.Kiroja cha mambo,ametiwa jeki na kule kushindwa vibaya kwa chama cha Leba katika uchaguzi wa Bunge la Ulaya.Kwani, hakuna muda wa kufanya mageuzi ya uongozi chamani.Kujiuzulu kwa Bw.Brown au kutiwa kwake munda , kusingeboresha nafasi za ushindi za chama cha Leba katika uchaguzi utakaofanyika kiasi cha mwaka kutoka sasa.Isitoshe, hakuna waziri-mkuu bora kuliko Brown kwavile, yule alietazamiwa sana kuvaa viatu vyake mfano waziri wa ndani Alan Johson au waziri wa nje David Miliband,kwa kutangaza ni watiifu kwa waziri mkuu Brown,hawakotayari kumuangusha..."

Ama tukigeukia uchaguzi wenyewe wa Bunge la ulaya uliopita majuzi,gazeti la Der Neue Tage laandika:

"Hoja za wafuasi wa bawa la kulia lenye siasa kali ambalo hasa lilitaka kujinufaisha kupata kura nyingi kwa kutokana msukosuko wa sasa wa kiuchumi,kuzidi ukosefu wa nafasi za kazi na hofu za kuongezeka wimbi la wahamiaji kutoka ngambo,ni za kurejesha watu nyuma.

Katika awamu hii ya utandawazi, kurejea mtindo wa kujilikinga na upepo wa nje, si suluhisho tena.Enzi ya kuwa na mamlaka kamili ya kitaifa kwa jicho la hatari zilizoukumba ulimwengu kama badiliko la hali ya hewa ,njaa Ulimwengu wa Tatu na matatizo yanayotokana na njaa hiyo, imepita.

Gazeti la Westfalische Nachrichten kutoka Munster linachambua juhudi zinazofanywa kuliokoa lisifilisike kampuni la ARCANDOR linalojumuisha duka kubwa la Karstad:LLaandika:

"Arcandor -shirika linalojumuisha kampuni la Karstad,Quelle na Thomas Cook, halitabaki katika mufumo wake wa sasa.Hata likipewa mkopo wa dharura kutoka serikali ya Ujerumani mjini Berlin,lisingeweza kwa muda mrefu kubakia lilivyo.Kwahivyo, Arcandor itiwe jeki tu,ikiwa fedha hizo za kuliokoa kufilisika zinaambatanishwa na masharti makali-mfano kulitenganisha na Thomas Cook."

Muandishi: Ramadhan Ali/DPA

Mhariri: M.Abdul-Rahman