1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchumi wa Ujerumani wakua zaidi.

Halima Nyanza14 Agosti 2010

Uchumi wa Ujerumani umekuwa zaidi katika eneo la nchi zinazotumia sarafu ya Euro katika robo ya pili ya mwaka 2010.

https://p.dw.com/p/OnXe
Waziri wa Uchumi wa Ujerumani Rainer Bruederle.Picha: AP

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Ofisi ya Takwimu mjini Wiesbaden, pato la ndani la Ujerumani limeongezeka kwa asilimia 2.2 ukilinganisha na robo ya kwanza ya mwaka huu.

Hali hiyo imefanya kukua kwa uchumi kwa kiasi kikubwa tokea kuunganika tena kwa Ujerumani miaka 20 iliyopita.

Commerzbank AG Deutschland Frankfurt
Moja ya benki nchini Ujerumani zilizonufaika na kukua kwa uchumi wa nchi.Picha: AP

Mkuu wa kitengo cha uchumi katika kampuni ya uwekezaji ya DekaBank, Holger Bahr amesema ukuaji huo umetokana sana na usafirishaji wa bidhaa nje na uwekezaji.

Aidha Pato la ndani la Ufaransa pia limeongezeka kwa asilimia 0.6 kwa kipindi cha miezi minne iliyopita, huku Uhispania uchumi wake ukiongezeka kwa asilimia 0.2.